Wizara: Akili Unde sasa kutengenezewa Sheria na Miongozo

Wizara: Akili Unde sasa kutengenezewa Sheria na Miongozo

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
762
Reaction score
1,007
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari nchini, imesema ili kukabiliana na kasi ya matumizi ya akili unde nchini, imekamilisha mkakati wa matumizi ya akili unde ikiwa ni katika kuelekea kuwa na miongozo kanuni na sheria zitakazo linda matumizi salama ya akili unde.
Akizungumza katika Jukwaa la Akili Unde la Tanzania ( Tanzania Artificial Intelligence Forum 2025), kaimu Mkurugenzi msaidizi kutoka Wizara ya mawasiliano na teknolojia ya Habari Mhandisi Bahati Zuberi, amesema mkakati huo utakuwa na masuala mbalimbali ikiwemo miongozo ya kupata watalaamu watakao simamia akili unde pamoja na masuala mengine ya uwezeshaji matumizi na kulinda haki miliki zitazo tokana na kazi zinazotengenezwa kupitia akili unde
Kwa upande wake Mkurugenzi wa tume ya TEHAMA Nchini Dokta Nkuwe Moses Masaga amesema, kutokana na maendeleo hayo ya matumizi ya akili unde ni wazi Tanzania ni lazima ijipange kutumia fursa pamoja na kukabiliana na changamoto zitakazo kuwepo kama vile kuweka sheria na kanuni ambazo hazitapotosha ama kuleta taharuki kwa jamii
Naye Mmoja wa watoa mada katika jukwaa hilo Jaji wa Mahakama kuu ya tanzania Dokta Adam Mambi amesema, Mahakama ikiwa ni mmoja wa taasisi zilizo nufaika na akili unde, inajivunia mafanikio iliyo yapata ikiwemo akili unde kusaidia kupunguza mlundikano wa mashauri huku akisisitiza kuongezwa kwa elimu ili kukuza uelewa wa jamii juu ya matumizi sahihi ya akili unde

Katika Jukwaa hilo kwa mara ya kwanza pia Tanzania imeendesha mashindano ya vijana Watalaamu wa kubuni na kutumia akili unde ili kutatua changanoto kwenye jamii
 
Okay ni jambo jema .

Lakini naona kama mpo kuzuia AI isitumike ipasavyo.
Kudhibiti AI.

Je serikali imejipanga je kuhakisha vijana wa ki TZ wananufaika na AI , ili na wao pia waweze kumiliki data centers zao mfano data centers za kilimo, uvuvi, Biashara, madini. Manufacturing industry and procees, medical and health centers, military, education etc.

Tahadhari hapa naona TZ ipo bize kuidhibiiti kiliko kuzitumia, shauri yenu
 
Back
Top Bottom