Wivu unavyoshusha hadhi mbele ya mpenzi wako

Wivu unavyoshusha hadhi mbele ya mpenzi wako

cuth_luxy

Member
Joined
Apr 29, 2013
Posts
15
Reaction score
21
Watu wengi sana wamekuwa wakidhani kwamba ukiwa na wivu katika mahusiano basi ni ishara ama ni alama mojawapo ya pekee kumuonesha umpendae kuwa una mapenzi ya dhati sana kwake. Sawa ni kweli yaweza kuwa unamaana hiyo, lakini kwa kwa upande mwingine unaweza ukawa unatengeneza picha yenye maana tofauti kwa mpenzi wako na mwisho wa yote ukaharibu kabisa mahusiano.

Kama kawaida ya safu hii ni kukumbushana na kujuzana mambo tofauti tofauti yanayohusu mapenzi, ili kudumisha mahusiano kati ya wawili wapendanao.

Leo tupate kidogo ufahamu kwa kujuzana ni jinsi gani wivu wako juu ya mpenz wako unaweza ukakusababishia kumpoteza huyo uliekuwa kuwa nae katika mahusiano.

1. Inaonesha ni jinsi gani una tatizo la ujasiri wa kujiamini mbele ya mpenzi wako.
Kuwa na wivu kupitiliza hicho ni kitu kibaya sana kinachompa picha mpenzi wako kuwa ni kiasi gani unashindwa kujiamini wewe mwenyewe. Kuna watu wengine wanaona ni heri kuwafungia ndani wapenzi wao ama kuongozana nao kila sehemu wanapokwenda kwa hofu ya kuibiwa.

Hii inatoa nafasi ya wazi kabisa kwa mpenzi wako kuweza kuona kwamba huna lolote na anaweza akatengeneza mawazo mengi sana yanayoishia katika suluhisho la kwamba mpenzi aliekuwa nae hajitambui.

Wivu ni muhimu lakini si kihivyo kuuzidisha kwa sana, mpe uhuru mwenzi wako afurahie uhuru wa mapenzi yako. Jiamini na tambua kwamba wewe mpaka kumpata huyo uliekuwa nae ni umefanya kazi kubwa sana na hakuna mwingine anaeweza kukupiku.

Kuonesha kwamba wewe ni mdhaifu kwa kumnyima uhuru mwenzio ni njia rahisi ya kumruhusu aondoke kutafuta mtu anaejiamini na atakaempa uhuru katika mapenzi.

2. Wivu unafuta uaminifu kati ya wapendanao.
Hali hii inajitokeza mara kwa mara katika mahusiano, na matokeo yake inasababisha malumbano ndani ya mapenzi. Kwa wivu wa mapenzi uliokithiri ndani ya mioyo ya watu wengi unakuta wanashindwa kuwaamini wapenzi wao hususani katika vitu vidogo vidogo tu.

Maswali tofauti tofdauti yanakuwa yanaibuliwa ndani ya wivu huu kulingana na mazingira tofauti mfano; Huyo aliekusalimia unamjua? Unamahusiano nae gani? Nani kakutumia huo ujumbe katika simu yako? Na maswali mengine mengi tu ambayo yanazua mtafaruku.

Sawa ni muhimu kufwatilia na kujua nyendo za mwenzi wako kama ni nzuri zizidi kuwa nzuri na kama nyendo ni mbovu basi kurekebishana yapaswa panapofaa lakini usiupe nafasi wivu wako kupoteza uaminifu kwa mpenzi wako. Ni hatari sana katika maisha ya mapenzi.

Kutokana na kukosa uaminifu kwa umpendae kamwe hutoweza kuhimili maisha ya mapenzi utabaki kulanda landa na hutofikia malengo ya maisha yako ya kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu, mwisho wa yote unaweza jikuta unaukwaa UKIMWI kutokana na kuruka ruka. Sababu ya wivu kila mwanamke ama mwanaume utaona hakufai.

3. Wivu unashusha heshima kwa wapendanao
Hapa tuwekane sawa, kutokana na vijitabia fulani ambavyo vinavyoibuliwa na mtu mwenye wivu kupita kiasi kwa mpenzi wake inasababisha heshima kati ya wapenzi hao kushuka na kuukaribisha ugonjwa mwingine wa utovu wa nidhamu.

Hali hii inapokuja kukomaa sasa kutokana na vichochezi vidogovidogo vya wivu ndipo visa vya hapa na pale vinapoanza kwa kuwa hakuna anaemuheshimu mwenzie. Malumbano hayakwishi kosa dogo tuu linakuzwa na kuwa kubwa na mara zingine inafikia hatua hata ya kurushiana ngumi.

Tatizo hili halipo tu kwa watu ambao ni wageni katika mahusiaono ya kimapenzi, bali ipo na inatokea sana hata kwa wanandoa.

Ni kitu kidogo tu yapaswa kila mmoja kujitambua na kujiheshimu vivyo hivyo pia afanye yampasayo kwa mwenzi wake. Katika safari ya mapenzi ukifanikiwa kudhibiti mipaka ya wivu basi utakuwa umefanikiwa kudhibiti moja ya chembechembe hatari sana inayosababisha mvunjiko wa mahusiano.
 
  • Thanks
Reactions: AMB
Wenye wivu wajinyonge mama, wenye wivu wajinyongeeee
 
mmm labda kwa watu wenye mtazamo kama wako ndo wanatakiwa wafanye kama wewe au kama jinsi ulivyo jaribu kueleza hisia zako binafsi mara baada ya kuona huyo ulienae ana wivu kwako so katika kubishana kwenu ukaamua utuletee na sisi ma great thinkers huku jf so i dont think if this is applicable generally
hata mungu anawivu i doesnt mean that hazi yake inapungua sasa haya mapenzi yasiyo na wivu hayo siyo mapenzi ila kujaribu na suala la wivu ni emotional
Siungani na wewe katika suala hili
 
mie kwangu wivu ni kipimo cha upendo wangu kwa mhusika

acha tu niwe zumbukuku
 
Ohh.........kumbe unazungumzia wivu uliokithiri/uliozidi, nimekuelewa.
 
wivu muhimu japo usizidishe utajuaje kama unapendwa
 
Wivu ni kidonda umeshiriki ugua pole - John Makini
 
Mtu asipokuwa na wivu na mimi aende akalale huko
 
Wivu una rangi ngapi?au ni kama bendera ya tanzania?
 
Kwenye mahusiano wivu muhimu ila usizidi kwan unapozidi unakuwa kero
 
Back
Top Bottom