Wivu-penzi la dhati au ulimbukeni? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wivu-penzi la dhati au ulimbukeni?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by eRRy, Mar 4, 2010.

 1. eRRy

  eRRy JF-Expert Member

  #1
  Mar 4, 2010
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 1,083
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135

  [​IMG]

  Kila mmoja anaweza kuwa maoni yake juu ya wivu, lakini naamni mtakubaliana nami kwamba, wivu katika mapenzi ni jambo lisilokwepeka hasa kwa sababu kubwa ya kuaminika inaonesha penzi lako la dhati kwake.

  Inadhihirisha kuwa, unampenda mpenzio na kwamba hauko tayari kwa namna yoyote ile kushea na mwingine. Ndiyo maana wanawake wengi hawataki kusikia suala la ukewenza! Hata kama jambo hilo limepewa baraka zote na dini au tamaduni zao, lakini wengi hawapendi kwasababu ya wivu.

  Lakini kubwa zaidi katika wivu ni kutokuwa tayari kusalitiwa na mpenzi wako hasa yule unayempenda kwa dhati na uliyemgharimia vitu vingi katika maisha yake. Usaliti unauma rafiki zangu, lakini chanzo cha yote hayo ni wivu. Unadhani kama hutakuwa na wivu na mpenzi wako, maana ya penzi lako itakuwa wapi?

  Ndiyo maana inashauriwa, kuhakikisha unamfurahisha sana mpenzi wako, kwasababu kama wewe usipofanya hivyo, akitokea mtu mwingine akapata nafasi ya kumfurahisha mpenzi wako, basi ujue umeshampoteza. Kiukweli kabisa, wivu una nafasi kubwa sana kwa wapendanao, ingawa wakati mwingine unaweza kuwa kero. Pamoja na hayo, wivu una umuhimu mkubwa sana kutoka na yafuatayo...

  UNAONESHA KUJALI KWAKO
  Sote tunaamini pasipo na wivu hata chembe, hapana mapenzi ya kweli. Kumuonesha wivu mpenzi wako ni kumjulisha ni kiasi gani unamjali na kumpenda na kwamba yeye ni mtu maalumu sana kwako.

  Jamani, mahali penye mapenzi yasiyo na wivu hata kidogo, panatia shaka! Mara nyingi majibu yake ni kutokuwa serious katika uhusiano huo au huenda kuna kupitisha muda tu na kwamba labda hakuna malengo. Lakini pia, inaonesha wazi kwamba penzi limeanza kuchuja.

  KUTHAMINI
  “Sio kama sikuamini dear, bali wivu wangu kwako ni katika kuuthamini uhusiano wetu, mimi na wewe ni umoja wenye thamani kubwa, tusiruhusu kuuchezea nje yetu!” Huu ni mfano wa ujumbe unaoonesha maana na nafasi ya wivu katika uhusiano wa kimapenzi.

  KUMKUMBUSHA
  Kauli au matendo yanayoashiria kumuonesha wivu mpenzio yanasaidia kwa kiasi kikubwa kumfanya mwenzi wako asijisahau katika jukumu la kulienzi penzi lenu hata akiwa mbali ya upeo wa macho yako.
  Kwa maneno mengine, utakuwa unamkumbusha kwamba yupo mtu ambaye anampenda na anamtegemea yeye katika maisha yake yote.

  UNALETA HESHIMA
  Kwa namna moja au nyingine, wivu pia huweza kukujengea heshima. Kwa mfano mume mwenye wivu na mkewe hujijengea heshima ya kwamba kweli anamjali na kumpenda mkewe lakini pia anaweka mazingira ya kutosumbuliwa kwa mke wake kwa kumjengea heshima yake kama mke wa mtu.

  HUBADILISHA TABIA
  Ukiwa na wivu, unaotokana na mavazi tatanishi anayopendelea kuvaa mpenzi wako, inaweza kusaidia kubadili tabia yake. Hivyo ni vizuri kumueleza mpenzio kuhusu nguo sahihi anazopaswa kuvaa kama mpenzi wa mtu ambaye yupo katika ndoa ya kuolewa. Naweka nukta.
   
 2. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #2
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wivu ni kipimo cha mapenzi mkuu,bila wivu hata maendeleo hakuna,hata enzi za adam na eva mungu alikuwa na wivu alipoona shetani ananyemelea wapendwa wake so WIVU ni mapenzi mkuu
   
 3. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #3
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Shida ni kuwa kuna wenzi wengine wanalalamika kuwa imekuwa too much! Asa tupeni maiwadha when is enough when is too much?
   
 4. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #4
  Mar 4, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Ulimbukeni!!!
   
 5. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #5
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Inategemea.Wakati mwingine wivu huwa ni kipimo cha penzi la dhati na wakati mwingine huwa ni kinyume chake,wizi tu mtupu.
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180

  How?:confused:
   
 7. kobonde

  kobonde Senior Member

  #7
  Mar 4, 2010
  Joined: Jan 6, 2010
  Messages: 154
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kama huna wivu basi humpendi mpenzio au mbinafsi unajifanya kama huna habari alafu akitoka unaanza kupekuwa kama unaibiwa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...