Magoya2000
JF-Expert Member
- May 7, 2017
- 641
- 1,266
Habari wana! Nimepitia mahusiano mengi lkn kitu ambacho kinakuwa kero kwangu ni hili suala la wivu. Mwanamke wangu ambaye nilifanya commitment naye alikuwa na wivu hatari kiasi hata ndugu akiniona nimesimama au naongea na ndugu anahisi namtibua. Kuna kipindi aliwahi kumtukana Boss wangu wa kike na kumkataza kuwasiliana nami. Boss wangu akaniambia huyo mwanamke hakuamini hivyo angalia sana atakuwa ni cheater mkubwa. Ukweli mwishoni nikagundua cheater. Sasa hivi nipo na mwingine nae wivu kama wote. Hataki niwasiliane na jinsia zozote za kike. Nimemchenjia kila mtu aishi atakavyo sio kubanana. Wivu ni upendo au mwenye wivu nae cheater tu? Tujadili!