Tunaendelea na takafuri. Ikitokea mtu wako wa zamani anaoa au anaolewa nenda harusini. Pale anapojibu ndio kumkubali mume/mke kama moyo wako haulii pa na moyo kuongeza kudunda tu-tu-tu basi jua hukuwahi kumpenda kabla. Hakika wivu ni kipimo thabiti cha mapenzi, kitumie vizuri kujipima kama unampenda uliye naye sasa ili msipotezeane muda. Kama hujui maana ya wivi soma hapa chini:
Wivu ni hali ya kumuona mwingine ni wako wewe tu hivyo kutotaka awe wa mwingine na hisia hii huendelea hata kama mtu si wako tena kutokana na ile historia ya u-sisi wenu iliyojenga umiliki wa pamoja wa hisia zenu na ndio maana kiukweli kwa watu waliopendana kwa dhati kabisa hakuna kuachana kikamilifu katika ngazi ya hisia ya wivu, kwa hiyo fanya maamuzi sahihi.