Wivu ambao sitausahau maishani

Wivu ambao sitausahau maishani

nyaggad

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
1,160
Reaction score
694
Habari wandugu,natumaini ni wazima,katika maisha yangu nilikuwa siamini kama wanawake huwa wanapenda kweli kutokana na historia yangu ya kutendwa.

siku mmoja nikiwa nyumbani kuna jirani yetu mmoja alikuwa mmpangaji wa nyumba ya karibu na kwetu ni mdada flani mwenye mtoto mdogo na anafanya kazi yake nzuri tu,alipigiwa simu na mtu nakuambiwa kuwa mme wake yupo maeneo flani anakula bata na mwanamke mwengine.

Wakati siku hiyo huyo mme wake alikuwa ameaga anasafiri kwenda mkoani sababu huyo mwanaume alikuwa dereva kwenye kampuni flani,cha ajabu yule mwanamke baada ya kupokea ujumbe huo akaamua kumpiga simu mme wake lakini simu haikupokelewa.

Alichoamua kufanya ni kwenda ndani kwake na baada ya mda,tukashangaa watoto wadogo wanakuja kumwambia mama kwamba,mama-x amejipaka mavi mwili mzima,mama alipoenda kuchunguza akagundua kuwa yule mwanamke alifanya hivyo kwa sababu ya hasira na wivu mkubwa kwa mme wake,baada ya mda mfupi watu walimpigia simu.

Mme wake na kumjulisha ndipo alipoamua kurudi haraka nyumbani wakayazungumza yakaisha,lakini yule mwanaume hakuacha ile tabia yake ya kuchepuka.

Siku nyingine tena yule mwanaume alichepuka na mke wake akapigiwa simu na watu wakamwambia,yule mwanamke baada ya kupewa taarifa hizo alikuwa ndani kwake akaamua kujimwagia mafuta ya taa mwili mzima na kujichoma moto

Baada ya muda mfupi majirani waliona moshi mzito ukitokea chumbani kwa yule mwanamke walipoenda kuangalia walimkuta yule dada ameungua vibaya sana,wakampigia simu mme wake na kumpeleka hospitali yule mwanamke, kwa bahati mbaya yule dada alikufa siku hiyohiyo na kuacha mtoto wake mmoja.

Kilichokuja kugundulika baadae kumbe yule mwanamke ndie aliyemtoa jamaa kwenye shida ikiwa pamoja na kumtafutia hiyo kazi ya udereva sababu huyo jamaa hakuwa na elimu kubwa,mke wake ndio alikuwa mkubwa,hii ni true story nilichojifunza.

"Usichukulie masihara mwanamke akikupenda kweli,kama ulitendwa huko nyuma usifikiri wote wapo hivyo wengine hawawezi kuishi bila wewe".
 
Habari wandugu,natumaini ni wazima,katika maisha yangu nilikuwa siamini kama wanawake huwa wanapenda kweli kutokana na historia yangu ya kutendwa,siku mmoja nikiwa nyumbani kuna jirani yetu mmoja alikuwa mmpangaji wa nyumba ya karibu na kwetu ni mdada mflani mwenye mtoto mdogo na anafanya kazi yake nzuri2,alipigiwa simu na mtu nakuambiwa kuwa mme wake yupo maeneo flani anakula bata na mwanamke mwengine na wakati siku hiyo huyo mme wake alikuwa ameaga anasafiri kwenda mkoani coz huyo mwanaume alikuwa dereva kwenye kampuni flani,cha ajabu yule mwanamke baada ya kupokea ujumbe huo akaamua kumpiga simu mme wake lakini simu haikupokelewa,alichoamua kufanya ni kwenda ndani kwake na baada ya mda,tukashangaa watoto wadogo wanakuja kumwambia mama kwamba,mama-x amejipaka mavi mwili mzima,mama alipoenda kuchunguza akagundua kuwa yule mwanamke alifanya hivyo kwa sababu ya hasira na wivu mkubwa kwa mme wake,baada ya mda mfupi watu walimpigia simu
Mme wake na kumjulisha ndipo alipoamua kurudi haraka nyumbani wakayazungumza yakaisha,lakini yule mwanaume hakuacha ile tabia yake ya kuchepuka siku nyingine tena yule mwanaume alichepuka na mke wake akapigiwa simu na watu wakamwambia,yule mwanamke baada ya kupewa taarifa hizo alikuwa ndani kwake akaamua kujimwagia mafuta ya taa mwili mzima na kujichoma moto baada ya muda mfupi majirani waliona moshi mzito ukitokea chumbani kwa yule mwanamke walipoenda kuangalia walimkuta yule dada ameungua vibaya sana,wakampigia simu mme wake na kumpeleka hospitali yule mwanamke, kwa bahati mbaya yule dada alikufa siku hiyohiyo na kuacha mtoto wake mmoja,kilichokuja kugundulika baadae kumbe yule mwanamke ndie aliyemtoa jamaa kwenye shida ikiwa pamoja na kumtafutia hiyo kazi ya udereva coz huyo jamaa hakuwa na elimu kubwa,mke wake ndio alikuwa mkubwa,hii ni true story nilichojifunza"usichukulie masihara mwanamke akikupenda kweli,kama ulitendwa huko nyuma usifikiri wote wapo hivyo wengine hawawezi kuishi bila wwe"

Mapepo ayo wala si kingine....ni kama wale wanaojikatakata wakikasirika
 
Nyinyi majirani na umbea umbea wenu wa kumpigia simu mumewe ndio mmechangia kifo cha huyo mama. Mara mmechungulia ndani kwake mara mnamwambia mumewe anachepuka daah huo mtaa sio wa kuishi hata kidogo
 
kujipaka mavi!!
kujilipua kwa mafuta ya taa..
sio wivu tena ni ukichaa
 
kafa na kamuacha mtesi wake akiendeleza bata na mumewe....😀
 
Duuh...Wivu ninao lakini sio wa namna hiyo..! Huyo alikuwa mgonjwa wa akili..!!
 
Ilikiwaje kila mwanaume anapochepuka mke wake anapigiwa simu kujulishwa? Mbona mimi nilikuwa nachepuka miaka 7 mke wangu hakuwahi kujulishwa na mtu yeyote? Hata hakuwahi kugundua au may be aligundua lakini hakuweza kupata uhakika halisi.
 
Duuh...Wivu ninao lakini sio wa namna hiyo..! Huyo alikuwa mgonjwa wa akili..!!

Inawezekana mkuu,maana hata mmi hiyo hali ili nitia wasiwasi,lakini mbona sisi tulikuwa tunamwona yuko poa2!!
 
ningekuwa na uwezo wa kumfufua ningefanya hivyo.


Then ningemtandika viboko vya maana kisha ningemuua na kumrudisha kaburini tena.
 
ningekuwa na uwezo wa kumfufua ningefanya hivyo.


Then ningemtandika viboko vya maana kisha ningemuua na kumrudisha kaburini tena.

Hahahhah,kwa nini mkuu?:what::what:
 
Back
Top Bottom