Wito:Zitto rudi bungeni kuonyesha uongozi

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Amani iwe kwenu.

Katika mapumziko yangu jjumapiliya leo nnimekuwa nnikitafakari ni kwa nini wabunge wetu kambi ya upinzani umepwaya,baada ya kupitia taarifa mbalimbali nikagundua yafuatayo;
1.Kutokuwapo Zitto Kabwe kumeleta ombwe la fikra na weledi wa hoja ikumbukwe tu katika kikao cha 2 bunge la 11 ZZK aliweza kueleza kwa ufasaha mapungufu ya hoja ya mpango wa serikali,hii ilisababisha KUB Mbowe,Lissu,Mbatia nk. kujisogeza kupiga picha na Zitto akiwa anahojiwa na wanahabari.
2.Ikumbukwe kwamba katika bunge la 10 ZZK alikuwa naibu KUB,kwa kiasi kikubwa alificha udhaifi wa KUB Mbowe pale mara kadhaa alipojitokeza na hoja zilizoitikisa serikali na hata kushawishi wabunge wa CCM kujiorodhesha kupiga kura ya kutokuwa na imani na serikali..mashinikizo yalisababisha mara kadhaa mawaziri kujiuzuru.

Kuna mengi ya kueleza ila itoshe tu kusema KUB kapwaya,hawezi kujenga hoja endelevu yenye kuweza kushawishi hadi wabunge wa chama tawala wamuelewe kuwa nia yake ni nini? Je mgomo wa bajeti ya PM umeweza kushawishi wabunge na wananchi kwa ujumla?..je hoja ni za kizalendo?

Nawasilisha.
 
Umuhimu wa Zitto utazidi kuonekana sana sana pale kwenye utata hasa unahitaji akili ya ziada(advanced thinking)
Zitto ni tegemeo hasà ktk kipindi hiki cha fikira pevu za upinzani.
 
Duu!!! Zito nae ameanza kuwekeza kwenye mitandao ya kijamii!!! Siku hzi naona siasa za kwenye mitandao ya kijamii zinalipa sana.
Haiwezekani narudi tena haiwezekani mtu mwenye akili timamu akaandika haya bila ushawishi nakataaa kabisa.
 
Kijana tatizo umezoea kutumuka ndio maana huna hoja ya kuchangia.
 
Umuhimu wa Zitto utazidi kuonekana sana sana pale kwenye utata hasa unahitaji akili ya ziada(advanced thinking)
Zitto ni tegemeo hasà ktk kipindi hiki cha fikira pevu za upinzani.
Ni muhimu sasa arudi...uwezo wake ni sawa na wabunge wote wa ukawa.
 
Back
Top Bottom