Rose Mayemba
JF-Expert Member
- May 7, 2012
- 721
- 1,017
Napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa watanzania wenzangu popote pale mlipo na haswa mijini, kuhakikisha ya kwamba tunarudi katika vijiji tulivyotoka kila tunapoweza. Sisi tulioko mijini na ambao tumeshuhudia moja kwa moja udhalimu wa Serikali hii ya CCM, tuna wajibu kwa ndugu zetu kufanya safari za kwenda huko vijijini ilimradi kuwatoa ndugu zetu kwenye giza totoro la kifikra ambalo chama tawala kiliweka, kinaweka na kitazidi kuweka miongoni mwa wananchi wengi hasa wa vijini. Ni wajibu wetu sisi ambao tumeweza kung'amua wizi huu unaofanywa na wachache wenye nafasi dhidi ya walipa kodi wengi ambao ndio walala hoi, kupinga na kuwasaidia hawa ndugu zetu wengine kupinga hali hii. Baada ya kuangalia clip ya video ambayo ilimuonyesha Nape akihutubia wananchi wa Makambako (wengi akina mama) na kushuhudia uongo unao enezwa na hawa jamaa kwa makusudi kabisa ilimradi kuwachanganya watu, nimeona nitoe wito huu. Ndugu zangu CCM ya sasa haina hata chembe ya uchungu kwa ajili ya wananchi wake zaidi ya kuendeleza propaganda zinazolenga kuisaidia kubaki madarakani. Kila kinachofanywa na serikali hii kinafanywa 'statergicaly' kuiwezesha CCM kubaki madarakani at the expense of the majority na sana sana kuhakikisha kwa makusudi kuwa raia wa kawaida haelimiki ipasavyo ilimradi waendelee kubaki gizani. Tukatae wizi huu. UFIKE MUDA SASA KILA MMOJA KWA NAFASI YAKE ASEME BAAAAS! YATOSHA! ENOUGH IS ENOUGH & TO HELL WITH CCM.
It begins with you
Comrade
Rose Mayemba
It begins with you
Comrade
Rose Mayemba