Wito wangu kwa wananchi wote majimboni kuhusiana na bajeti ya mwaka 2012/2013 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wito wangu kwa wananchi wote majimboni kuhusiana na bajeti ya mwaka 2012/2013

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ruhazwe JR, Jun 25, 2012.

 1. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  UTANGULIZI
  Nawasalimu wanajamvi wote na wapa poleni ya majukumu ya kusaka mkate wa kila siku.

  Leo nimeona ni vema kutoa wito kwa wananchi wote kuhusiana na Bajeti ya serikali ya Mwaka 2012/2013.Wito wangu unakuja katika kipindi ambacho Bunge la Jamuhuri wa Muungano lipo bize katika kupitisha bajeti,Bajeti ambayo kwangu haina matumaini ya kukabiliana na hali ngumu ya maisha ya wananchi walionayo kwa sasa.Ninaposema hali ngumu ya maisha ni kwa wale wote ambao si mafisadi.

  WITO
  Wito wangu ni kwamba wananchi wote hasa wa majimboni tuungane kwa pamoja bila kujali itikadi za Vyama vyetu,Kuungana pamoja katika kujua ni mbunge gani akiwa Bungeni(Bunge linalo endelea kwa sasa)amethubutu kuchangia kwa namna yoyote ile kupita kwa bajeti hii ambaye haitakua na tija kwa wananchi.baaada ya kuw Tumewwjua tuungane pamoja kuwangoja kwenye majimbo yetu tuandamane kuwafata kuwataka kwamba ni Kwanini wasiwajibika kwa kujiudhuru nafasi zao za Ubunge kwa kuwa wameshibdwa kuwajibika kwetu wananchi kwa kupitisha Bajeti ambayo ni Takataka kwetu wananchi na ni dili kwa wajanja wachache,ambao ndio wanatufikisha katika maisha magumu ya sasa.

  Nasema hivi kwakua wabunge wanachangia kupitisha madudu ambayo hayana maslah kwa sisi wananchi isipokuwa yana maslah kwa vyama vyao wanavyotoke na yana maslah kwa serikali legele ambayo ni dhaifu kwa kila lolote linalotoke.

  Sitaki kamini kuwa Wabunge wetu hawajui nini wananchi tunataka,Sitaki kuaminin kuwa wabunge wetu hawajui hali ngumu ya maisha tuliyonayo wananchi.Ikumbukwe kuwa Mwanachi ndio bosi wa Mbunge,Mbunge bosi wake si serikali,wala chama anachotoke,Mbunge bosi wake ni yule ambaye amempeleka bungeni hivyo anapaswa kujua nini mwananchi anataka na ndicho anapaswa kupitisha Bungeni.

  Serikali imetia pamba mskioni hataki kusikia kilio cha watanzania walio wengi,Serikali imevaa miwani ya Mbao haitaki kuona mateso na taabu tuliyo nayo wananchi wake,kufanya hivyo nathubutu kusema serikali inakiuka katiba kwa kuto kuja na Bajeti ambyo si bajeti yenye mwendelezo wa bajeti iliyopita ya 2011/2012 pamoja na maadhimio yaliyopitishwa na Bubge kuusu mikakati ya maendeleo ambayo labda ingeweza kubadilisha maisha haya magumu kwa Watanzania.Kwa mujibu wa katiba Ibara ya nane,mwananchi ndiye mwenye mamlaka dhidi ya serikali.

  Naomba sana wananchi wote tuungane kuwafata wabunge wetu ambao kwa namna moja au nyingie watakua wamethubutu kusema "Naunga mkono Bajeti",lazima wabunge hawa wawajibike.

  HITIMISHO

  Najua kuna watu watakuja na hoja za vyama,Hoja yangu ni Bajeti mbovu kwa mwanachi na uwajibikaji wa wabunge katika kuipitisha Bajeti.Kumbuka Dunia ni yako,Tanzania ni yako,chagua kudai haki bila woga kwkua Haki haiombwi bali hudaiwa.

  Nawasilisha
  Ruhazwe JR
  jimmyjrtz@yahoo.com
   
 2. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  kiongozi!binafs nimekupata,lakini tukiamua kufanya hivyo kama usemavyo watajikuta karibia wabunge wote wale wa CCM ndio watakao kumbwa na mkasa huu.ambao wengi wanakua na maneno makali ktik kuchangia alafu mwishoni anasema "naunga mkono bajeti".Wakati ndio sasa,bora mie mbunge wangu Mdee hajaiungamkono lakn ntakwenda kwa mhe iddi azan kupinga na ntakwenda hadi kwa zungu kupinga,andaeni utaratibu tu
   
 3. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #3
  Jun 25, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wakati ndio sasa huu ni wakati wa kutokubaki nyuma katika kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi,Tukiamua tunaweza!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
Loading...