Wito wangu kwa vijana, wazee

Manyerere Jackton

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
2,436
4,429
Ndugu zangu, kitambo sasa sijashiriki mijadala mingi kwenye uwanja wetu mwanana wa JF. Nilikuwa masomoni. Kwa mapenzi yake Mola nimehitimu vema Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) nikiwa nimechukua kozi ya Mass Communication.

Nimeona niandike haya ili kuwatia shime wana JF, hasa wenye umri wa utu uzima kama mimi, kwamba kusoma ni kitu kizuri sana. Kabla ya kusoma kozi hii nilidhani najua mengi- nilipoingia darasani nikabaini nilikuwa si lolote wala chochote.

Nakumbuka miaka kama 10 iliyopita mwana JF mmoja alinitandika dongo akisema, "Manyerere rudi shule kasome, umri bado unakuruhusu".

Nikiri kuwa maneno hayo yalinichoma na kwa kweli yalinisukuma nirudi shule. Kwa wale wenye umri mdogo nawashauri sana sana tafuteni shule muongeze maarifa.

Kusoma kuna raha zake hasa elimu hiyo inapokuwa na tija kwa jamii tunamoishi. Nawaomba sana vijana someni. Mungu awabariki.
 
Back
Top Bottom