Wito wa Shigongo wa Vijana wa UVCCM

UVCCM mbali ya kuhimizwa kuzungumzia mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya chama chao, ijapokuwa kupitia kodi za wananchi, lakini pia wanapaswa kutoa ushauri mzuri kuhusu changamoto zinazowakabili vijana wenzao, hasa kwa sasa kundi la machinga.

Ni lazima watambue ya kuwa kundi hili linaloanza kubagwazwa hivi sasa, lilikuwa ni kundi pendwa kwa mfalme aliyepita. Hisia ya kundi hili lilionekana wazi hata katika mazishi yake.

Katika miji ulipopita mwili wa marehemu mfalme aliyepita, vijana hawa walijitokeza kwa wingi na walifunga biashara zao na kwenda kumuaga. Vilio na machozi viliwatoka hadharani na huku wakipaza sauti na kumuita mpendwa wao "JESHI"

Madam President ameshika madaraka yapata miezi 6 tu iliyopita. Ni mapema sana kuanza kuainisha kwa sifa na kuabudu mafanikio yake. Ni vyema UVCCM wakajikita katika kutafuta suluhu katika changamoto zinazowakabili vijana wa sasa, hasa katika maeneo ya ajira, mitaji ya biashara, stadi za maisha na kuaminika zaidi katika masuala ya uongozi.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…