Wito wa Shigongo wa Vijana wa UVCCM

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
2,357
2,000
NAWAANDIKIA kuwahimiza vijana wa CCM kuipigania CCM na serkali yake popote mtakapokuwa, iteteeni CCM, mtetee Rais wetu Samia Suluhu Hassan, semeni mema yanayofanyika na awamu ya sita kwa nguvu zote.

Msiposema nyinyi watasema maadui zetu, ambao kamwe hawatasifia isipokuwa kuwaaminisha watu kwamba hakuna kilichofanyika. Vjana wa CCM jielimisheni, fanyeni utafiti Kisha muingie kwenye mijadala na mjenge hoja za nguvu kwa kusema ukweli dhidi ya upotoshaji.

Kila kijana wa CCM atafute askari 5-10 waaminifu wa mtandaoni (online soldiers) watakaojitolea kupigania CCM na serikali yake mitandaoni ambako ndiko hasa vita ilikohamia, huko ndiko watu walipo na adui analifahamu hili na anapigana kufa ma kupona, sisi tumetulia ama tunapigana mmoja mmoja kinyonge!

Hapana, sasa imetosha! Vijana wa CCM mna nguvu kubwa, unganeni, pambaneni kwa maslahi mapana ya taifa letu:hii ni dhamana ambayo Chama chetu kimekabidhiwa, mna wajibu wa kulinda taifa hili, TETEENI CCM NA SERIKALI YAKE KWA NGUVU ZOTE, BILA HOFU WALA VURUGU BALI KWA HOJA!

CCM OYEEEEEE!

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.

Together we strong,

Separated we're WEAK!

~Eric James Shigongo.
UVCCM mbali ya kuhimizwa kuzungumzia mambo mazuri yanayofanywa na serikali ya chama chao, ijapokuwa kupitia kodi za wananchi, lakini pia wanapaswa kutoa ushauri mzuri kuhusu changamoto zinazowakabili vijana wenzao, hasa kwa sasa kundi la machinga.

Ni lazima watambue ya kuwa kundi hili linaloanza kubagwazwa hivi sasa, lilikuwa ni kundi pendwa kwa mfalme aliyepita. Hisia ya kundi hili lilionekana wazi hata katika mazishi yake.

Katika miji ulipopita mwili wa marehemu mfalme aliyepita, vijana hawa walijitokeza kwa wingi na walifunga biashara zao na kwenda kumuaga. Vilio na machozi viliwatoka hadharani na huku wakipaza sauti na kumuita mpendwa wao "JESHI"

Madam President ameshika madaraka yapata miezi 6 tu iliyopita. Ni mapema sana kuanza kuainisha kwa sifa na kuabudu mafanikio yake. Ni vyema UVCCM wakajikita katika kutafuta suluhu katika changamoto zinazowakabili vijana wa sasa, hasa katika maeneo ya ajira, mitaji ya biashara, stadi za maisha na kuaminika zaidi katika masuala ya uongozi.

Sent from my Nokia 2.3 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom