Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,689
- 119,326
Wanabodi,
Tangu baada ya Nyerere, na mtindo ule wa vitendo bila kuchelewa na utoaji wa maamuzi magumu, Watanzania walimisi sana maamuzi ya aina hii kwenye utawala wa Mwinyi, Mkapa na Kikwete, hivyo sasa wanashangilia sana kila maamuzi ya utumbuaji wa majipu wa papo kwa papo ya rais wetu, Dr. John Pombe Magufuli, kwa kufanya vitendo bila kuchelewa, kwenye utumbuaji. Hili lilifanyika kwenye Utumbuaji wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, alilalamikiwa kwenye kadamnasi ya watu pale Kigamboni siku ya uzinduzi wa Daraja la Kigamboni!, JPM akauliza, tumfanye nini?. Watu wakajibu, "Tumbua...!" huku wakishangilia, na kweli JPM akatangaza hapo hapo, kuanzia sasa.. , umati ukalipuka kwa kushangilia kwa furaha!. Kitendo cha kiongozi Mkuu wa nchi, kufanya maamuzi ya papo kwa papo kwenye mikutano ya hadhara, ili kuwafurahisha watu, kisiasa hii inaitwa "populism", na kumfanya huyo kiongozi kuwa, "a populist leader" kiongozi anayependwa na watu, na mtindo huu wa uongozi unaitwa "Populism", kiongozi anayetumia mfumo huu wa populism kukubalika kwa umma, anaitwa "a populist leader" hivyo rais Magufuli is a populist leader.
Tukio kama lile la kumtumbua Mkurugenzi wa Jiji, jana limefanyika tena kwa JPM kumfukuza kazi Katibu Tawala Mkoa wa Mwanza, Dr. Faisal Issa, kwa kumtumbua, baada ya kupokea taarifa ya utovu wa nidhamu wa Katibu Tawala huyo kumkwida Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye kikao. Inasemekana, RC baada ya kukwidwa, ndie alimpigia simu the Big Boss, na the Big Boss acted promptly by firing RAS!.
Enzi za Nyerere, alikuwa akipokea taarifa tuu ya wale 'watu wake', Nyerere ali act bila kuchelewa, kwa kupeleka taarifa ya kufukuzwa kazi, kwa Radio Tanzania, wakati huo, Mzee David Wakati,(RIP) akiwa Mkurugenzi, na kutokana na unyeti wa taarifa yenyewe, wakati mwingine, ilimlazimu Mzee David Wakati mwenyewe, kuingia Studio na kusoma Taarifa ya Habari ya saa mbili usiku ya siku hiyo!. Ilifikia mahali baada ya zile ngoma za Mzee Morisi Nyunyusa, ikisikika tuu sauti nzito:"HII NI TAAIFA YA HABARI KUTOKA RADIO TANZANIA, DAR ES SALAAM, MSOMAJI NI DAVID WAKATI...", baba anatoa amri wote kimya ... maana kuna jambo kubwa litatangazwa!.
Mtindo huo wa timua timua wakubwa ya Mwalimu Nyerere uliitwa 'Fagio la Chuma'.
Kuna msemo unasema, kila zama na zama zake, mtindo huu wa kufukuza watu ghafla kwa enzi zile za Nyerere, ulikuwa sawa kwa sababu ndizo zilikuwa zama zake, lakini kufufuliwa kwa mtindo huu kwenye zama hizi za sasa za "the world of information age", japo watu wanashangilia, lakini sio mtindo mzuri hata kidogo.
Enzi zile mtindo wa utawala ulikuwa ni Top-Butom, unaanzia juu kwenda chini, enzi hizo mkubwa ndio kila kitu, akisema, amesema, wa chini wote ni utekelezaji tuu bila hata kuuliza!. Hivyo enzi za Nyerere, rais Nyerere ndio alikuwa kila kitu!.
Enzi hizo, kulikuwa na amri inayoitwa "Presidential Preventive Detention Order" inayompa mamlaka rais (baada ya kuelezwa na watu wake), kumtia ndani yaani "kizuizini" mtu yoyote, kwa kipindi chochote, bila kuelezwa chochote, na bila kufikishwa kwenye mahakama yoyote! and it was ok!. Kwa zama zile Mwalimu Nyerere aliitumia sana tuu amri hii na kumfanya kuwa ni mtu anayeogopewa sana hadi na mabeberu!.
Japo sheria yenyewe bado ipo, ila kwa sasa rais hana tena mamlaka ya kujiamualia kumtia mtu yoyote ndani kwa muda wowote bila kumweleza lolote au bila kumfikisha mahakamani, sheria inatamka yoyote atakayewekwa kizuizini na rais wa JMT, kwanza ana haki ya kuambiwa ni kwa nini, au kwa kosa gani, pili ni lazima afikishwe mahakamani ili mahakama ndio iridhie mtu huyo kushikiliwa ndani ya saa 24, na sii zaidi ya siku 14!, kisha mtu huyo anayo haki ya kupata utetezi wa kisheria, na kupiga kuwekwa kizuizini, hivyo zama zimebadiliki, kwa sasa hadi amri ya rais zinapigwa mahakamani, hivyo sasa rais sio kila kitu, bali haki ndio kila kitu!
Katika suala la Dr. Feisal Issa, kwa wale tunao mfahamu, Huyu jamaa ni wa kabila la Wairak, Jamii za Wambulu, wa Barbaig, Warangi, Wanyaturu, baadhi yao wana nywele kama za Kisomali, kama Aden Rage, au Hussein Bashe. Hawa jamaa ni watu wenye hasira sana wanapochokozwa, na hawapendi kabisa kufananishwana na Wasomali!
Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, kama ni kweli RC Magesa Mulongo mbele ya kadamnasi ya kikao cha kamati ya Ulinzi na Usalama "We Msomali", na kumsema Dr. Feisal sio Mtanzania bali ni Msomali, by nature ya nafasi ya Mkuu wa Mkoa, hii inaitwa Bullying of the highest order!, hivyo kitendo cha Dr. Feisal kwenda kumkunja Mulongo kisheria kinaitwa acting under provocation, alitukanwa, alibaguliwa na kudhalilishwa utu wake kwa kuwa degraded mbele ya watu, ni human nature kwa binadamu ku react kwa self defence, under provocation hivyo kama kuna kitu chochote karibu, anaweza kukishika na kukupiga nacho au hata kukuua, na bado mahakama ikamuachia huru kama ikithibitishwa beyond reasonable doubt kuwa his actions were done under provocation!
Japo nakubaliana na dhana kuwa hapo tulipofika Tanzania inahitaji kiongozi wa dictatorship ya type hii ya Magufuli, na JPM anafit sana kuwa ndiye kiongozi anayehitajika sana kwa Tanzania ya sasa ili mambo yaende, na type ya maamuzi hayo, ndiyo yanayotakiwa kwa sasa ili tuweze kusonga mbele!, nakubali inawezekana kabisa Magufuli anafanya the right thing but in a wrong way!
Hata kama ni kutimuliwa, yes watovu wa nidhamu wote watimuliwe, lakini utimuaji huu ufuate haki, na sio kwa papara kama hizi tunazoshuhudia sasa bali ufanyike baada ya tafakuri ya kina na kujiridhisha, na asiishie hapo kwa Dr. Faisal Issa, bali Magesa Mulongo naye pia alipaswa kutimuliwa vile vile ili kumuepushia Magufuli na maamuzi ya double standards!. Mkuu wa Mkoa kamtukana mtu, kiongozi mwenzake, mbele ya watu, aliyetukanwa, amedhalilishwa, and was acting under provocation, akamkunjwa shati bosi wake, anayefukuzwa ni aliyetukanwa tuu!, aliyetukana kaachwa kwa sababu ni mkubwa!. Hapa tumedeal na matokeo tuu na kukiacha chanzo!
Inasemekana this is not the first time kwa RC kumdhalilisha RAS, na wana ugomvi binafsi wa mambo fulani, naomba nisiutaje, ukawa ni umbea!, it's not right kwa rais wetu kufanya maamuzi ya haraka kwa kila umbea anaopelekewa na wale "jamaa zetu", kuna watu wataonewa bure, karma ikaja kufanya malipizi!
Amini msiamini tukiendele hivi hatufiki!. Tanzania hatuhitaji maamuzi ya zimamoto huku tukiimbiwa nyimbo za shangwe, sifa
na mapambio, tunahitaji mfumo wa utendaji tofauti na ule utendaji wa mazoea! kwa kujenga systems, mifumo imara na madhubuti, na sio kutegemea mfumo huu wa one man show tunayoishuhudia!
Mungu Ibariki Tanzania.
Wasalaam.
Pasco