Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 57,103
- 128,723
Wanabodi,
Huu ni wito kwa wana tasnia ya habari, "Moja shika sii kumi nenda rudi " and "if you can't get what you want, then just take what you get", baada ya kusainiwa kwa sheria mpya ya habari, sasa tuzivunje kambi zote pingamizi, tutoe ushirikiano kwa utekelezaji wa sheria hii mpya.
Tumpe ushirikiano wa kutosha waziri wa Habari, atengeneze kanuni bora, aunde Baraza bora la ithibati ya waandishi, tuunde Baraza huru la habari litakalo shehenezwa manguli wa tasnia hii, halafu yale yote yenye ukakasi, yatachomolewa moja baada ya jingine na yale mazuri yatachomekwa moja baada ya jingine kupitia marekebisho ya sheria hii.
Nawaombeni sana tusimlaumu rais Magufuli kuusaini huo muswada kwa haraka, kwa sababu uharaka huo ni uthibitisho wa kutoingilia mhimili wa Bunge, maadam wabunge ambao ndio wawakilishi wetu Wameridhia na kuipitisha hiyo sheria, who is he, asiisaini? !.
Sii wengi wanaoujua kuwa kuwa iwapo bunge limetunga sheria, Rais ni lazima aisaini, na asipo isaini basi anapaswa au kulipigia magoti bunge lirekebishe kile rais anachotaka, Bunge likingomea, rais anakuwa hana jinsi bali anapaswa kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu mpya wa wabunge tuu! .
Sasa ukiangalia jinsi wananchi walivyopigika kwa ukata, njaa na msoto, ukijumlisha na umasikini wetu uliotopea, hili bunge la chama dola lukivunjwa leo na uchaguzi kuitishwa, no one is sure to return, sasa nani yuko tayari kwa bura yangu njema kubadili kwa rehani, au kuchezea shilingi chooni?!, bora alivyosaini.
Sheria hii mpya ya habari ni kama tuu katiba mpya, Watanzania walitaka katiba bora, lakini wakapatiwa bora katiba. Ndivyo hivi kwa miaka 20, waandishi tumelilia sheria bora ya habari, tumeletewa bora sheria, tuikubali, tuipokee, tuitekeleze kwa roho safi.
Hata wewe kama kuna kitu fulani kizuri ulikihitaji lakini ukakikosa, ukafanikiwa kupata kingine kidogo, kibaya, then kukubali tuu hicho kidogo na uwe na shukrani kwa kidogo ili upatiwe kikubwa.
Mfano mzuri ni mimi mwenyewe, nilitamani sana kuendesha Range Sport, lakini kwa mishahara ya sisi watangazaji wa zamani enzi za RTD, uwezo wetu ni kumiliki boda boda, nilinunua boda boda na ndio usafiri wangu siku zote mpaka boda boda iliponifanya vibaya, sasa niko kwenye bajaj, ila kila nikipishana na Range Sport, naitazamaa na kusmile kimoyo moyo huku nikijisemea gari kipenzi changu, halafu nashukuru kwa bajaj yangu, vivyo hivyo waandishi tushukuru kwa sheria hii.
Maoni yangu yanafuata.
Sheria hii mpya ya Habari ni ina deal na print tuu, broadcast iko wizara nyingine, mamlaka nyingine na sheria nyingine chini ya TCRA, kule unajisajili kwa TZS 1.M, kisha unapeleka unlimited number ya waandishi wa social media ambao hawana cheti chochote!, wote wanapewa press cards tunakutana ulingoni!
Bodi ya Ithibati iangalie fani ya utangazaji ni vipaji na sio vyeti, na pia hii fani mpya ya social media, kuwataka watangazaji wote na watu wa social media wawe na diploma ni kuwaonea bure!.
Paskali:
Mwandishi ni mwandishi/mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea.

Kwa mujibu wa sheria hii, kama nilivyosema mwanzo, hii ni ile Newspaper Act ya 1976 iliyoboreshwa, hiyo bodi ya Ithibati isiwe rigid kusajili waandishi wa habari wa diploma tuu.Mapendekezo Yangu Kwa Muswada wa Habari 2016.
Nimeyaandikwa kwa Kiswahili, kama heshima na kuenzi Lugha yetu adhimu ya Kiswahili, lakini ile watu wengi zaidi waweze kufaidika na maoni haya.
Utambulisho.
Mimi Pascal Mayalla ni Mwandishi wa Habari wa kujitegemea kwa kujitolea ( Independent Media Practitioner and not a Freelance Journalist)
Tofauti kati ya Freelance Journalist, na independent journalist, Freelance ni mwandishi anayeandika na kulipwa na media kwa kazi hiyo ya kuandika kwa kadri habari zake zitakavyotumika, na hukitegemea kipato cha uandishi wa habari kuendesha maisha yake.
Independent Journalist ni mwandishi anayeandika kwa mapenzi yake tuu, kwa kujitolea, na husambaza habari zake bure kwenye media, bila kutegemea kulipwa chochote na media hizo. Huyu ni mwandishi mwenye shughuli nyingine anayoitumia kupatia kipato kuendesha maisha yake, lakini anaandika kwa mapenzi tuu.
Mimi Pascal Mayalla nilianza uandishi wa habari Mwaka 1990 kwa kuajiriwa Radio Tanzania Dar es Salaam, RTD kama Mtangazaji fresh from school, nikiwa RTD nilisomea Diploma ya Uandishi wa Habari kutoka Chuo Uandishi wa Habari, TSJ 1992-1994.
Mwaka 1995 Televisheni zilipoanza, niliacha kazi RTD na kujiunga na kituo cha Televisheni cha DTV nikawa ni Mtangazaji.
Mimi ndiye mtangazaji wa kwanza wa vipindi vya TV Talks Shows Programs kwa kuanza ni kipindi cha Mada Moto, na baadaye Kiti Moto.
Mwaka 2000 nilijiunga na TBC na mwaka 2002 nilifukuzwa kazi TBC kosa ambalo mpaka kesho silielewi, ila nikaanzisha kampuni ya Uandaaji wa vipindi vya redio na Televisheni, ya PPR, ambapo imeisha iingizia TBC zaidi ya shilingi bilioni moja, hivyo hata ningeendelea kuwa mtumishi wa TBC nisingeweza.
Sio kila kufukuzwa kazi ni balaa au majanga, kufunguzwa kwingine ni Blessing in Disguise” kwani kufukuzwa kwangu kazi TBC, ile 2002, kulinipatia fursa ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mwaka 2003-2007 na kusomea shahada ya Sheria , LL.B.
Hivyo natoa maoni yangu kama
1. Mwandishi wa habari mzoefu
2. Mmiliki wa Chombo cha Habari
3. Mwanasheria
Pascal Mayalla
Press & Public Relations (PPR)
Mob. 0784 270403
E-Mail: pascomayalla@gmail.com
Part 1: Preliminary Provisions
Short Titles.
Kuna makundi muhimu yameachwa kwenye kundi la nani ni mwandishi wa habari, waandishi, nashauri, zaidi ya Freelance Journalist,
Waongeze Independent Journalists, ambao sio ma freelancer, hawategemei media.
Pia waongeze Media Contributors, hawa ni professional people wenye professions nyingine, lakini wanaandika in depth kuhusu makala mbalimbali.
Waongeze Specialized Journalist -hawa ni waandishi wenye professionals nyingine ambazo ni specialized mfano medicine, nursing, account, environmental, scientists, geographic, tourism, etc, ambao wanaandika as specialists.
Waongeza Independent Production Houses,
Muswada utenganishe Public Media na Government Media.
Public Media ni vyombo vya habari vya umma hata kama vitagharimiwa na serikali kama ilivyo TBC na RTD zina wajibika kwa umma kupitia bodi zake zinazojitegemea, serikali inazighaimia tuu na kuziangazia tuu, eyes on, hands off! Na sio kuziingilia kama ilivyo kwa BBC.
Government Media ni Vyombo vya Habari vya serikali, kama Daily News, Idara ya Habari Maelezo na Government Gazette vinawajibika kwa serikali with eyes on, hands on.
Muswada huu unaonekana kujihusisha zaidi na print media, broadcast media, imeachwa nje, ndio maana kuna journalists na editors tuu, wakati kwenye broadcast kuna producers, cameramen, presenters, etc, siwaoni humu, mtu kama ni producer kumuita journalist ni kumshusha, kama jaji kumuita wakili.
Huwezi kuyaweka mambo yote ya media kwenye kapu moja na kuwalazimisha wawe na vyeti a, mfano broadcasting kuna watangazaji ambao ni talents na sio vyeti , kuna technical, kuna watu wa sound, light, huwezi kulazimisha wawe na diploma!.
Part 2: Information services.
Ibara ya 5: Kwenye majukumu ya Director of Information Services, ameonyeshwa atasajili print media pekee, lakini sio broadcast media , its high time tuunganishe vyombo vya habari vyote chini ya mwamvuli mmoja.
Ibara ya 6: Kwenye ownership, kumetambuliwa makundi mawili tuu ya Public na Private, kwenye kundi la public, imetajwa serikali, hapa nasisitiza tena, kuwe na makundi matatu na sub kundi moja
1. Government Media
2. Public Media
a. Public Media Owned By The Government
b. Public Media Owned by The Local Government
c. Public Media Owned by Communities (kama ilivyo kwa public companies)
3. Private Media
Mfano kwa hali ilivyo sasa, TBC inajulikana kama ni chombo cha habari cha serikali, kiukweli TBC ni chombo cha habari cha umma, kinatakiwa kugharimiwa tuu na seikali lakini kuuhudumia umma wote wa Tanzania kama ilivyo BBC.
Ibara ya 7: Kwenye Oligation nazo ziwe vile vile,
Government Media itoe taarifa za serikali
Public Media, obligation ya kwanza iwe ni kutoa public information bure zikiwemo public information programs. Public media iwe channeli mbalimbali, moja ya chaneli hizo iwe ni public information channel ambayo itatoa huduma bure, na kama ni kuweka gharama, ziwe ni service fee only and not for profit.
Mfano kwenye shughuli zozote muhimu kwa umma, kama maadhimisho, au maonyesho wa Saba Saba, Nane Nane na maonyesho mengine au shughuli nyingine yoyote yenye public interest, public media itoe huduma za matangazo bure. Najisikia uchungu sana TBC kucharge gharama kubwa ya shilingi milioni 1 kwa dakika 10, mkulima gani atamudu kutangaza ubunifu wa kilimo utakaolisaidia taifa hili kwa gharama hizo?. Najikuta naendesha kipindi cha Wakulima Nane Nane, badala ya kuonyesha mambo ya kilimo, tunaonyesha mambo ya wenye fedha wanaomudu matangazo hayo.
Viwekwe viwango vya gharama vya chini kwenye public media.
Hitaji la Vyeti Vya Kitaaluma Kwa Waandishi wa Habari.
Sheria mpya inataka mwandishi wa habari lazima awe na angalau diploma ya habari.
- Kwanza mimi kama mwandishi wa habari mkongwe, naunga mkono hoja hii kwa asilimia 100% kwa 100% ili kujenga heshima ya tasnia ya habari as a professional, kama walivyo wanasheria, madaktari, maengenea na any professional nyingine zote.
- Uandishi na utangazaji ni kipaji, lakini pamoja na kipaji, ili mtu awe mwandishi au mtangazaji lazima apite shule ya habari kupigwa msasa angalau hata certificate.
- Hakuna popote kwenye muswada kumeandikwa mwandishi lazima awe na degree. Lakini kwa sababu muswada unaanzisha accreditation board itakayowasijili waandishi, sisi waandishi wakongwe mimi nikiwa ni mmoja wao ambao tunapendekeza accredited profession journalist lazima wawe na shahada ya Chuo Kikuu ili kujenga heshima kama tasnia ya sheria.
- Kwenye tasnia ya sheria , japo kuna certificate, diploma na degree, mtu huwezi kuwa advocate hadi kwanza uwe na degree, kisha uende Law School ndipo usajiliwe na mahakama kuu kama wakili.
- Hata uwe na diploma mia, hata uwe na Ph.D ya sheria, kama huna LL.B huwezi kuwa wakili. Kama kwa wanasheria hili limewezekana kwa nini kwa waandishi lisiwezekane? .
- Hao wenye certificates watasajiliwa kama assistant journalists lakini sio professional journalist. Hao wenye diploma watasajiliwa kama ordinary jourlists lakini sio professional journalist. Na watakao sajiliwa kama accredited profession journalist wawe ni wale tuu wenye degree holders tuu!.
- Hii sasa ni fursa ya kuijengea heshima tasnia ya habari kama taaluma yenye kuhushimika kama taaluma ya sheria, na wanahabari tuwe kama ilivyo kwa wanasheria, ili mtu awe wakili, lazima kwanza apate shahada ya sheria, LL.B, wale wengine wote wenye certificates au diploma za sheria, ni ma para legal na sio mawakili. Hivyo Waandishi pia wagawanywe makundi, professional accredited journalist ili kuwa Accredited Journalist lazima kwanza uwe na a university degree ya journalism or related field.