Wito kwa tanesco

Chona

JF-Expert Member
Mar 8, 2010
523
360
DSC_0069_40f10.JPG

Wengi mtakuwa mnatambua eneo hili. Eneo hili lipo kati ya kituo cha daladala cha Sayansi na Kituo cha Bamaga.
Lengo langu kuu ni kuwafahaisha wahusika wa Tanesco kuwa kuna nguzo moja ya umeme maeneo hayo nyanya zake nadhani hazipo sawa. Kila ninapopita hasa kama kuna foreni utasikia sauti kama ya cheche ikitoka kwenye nguzo moja wapo. Kumbuka hilo ni eneo ambalo huwa na foreni wakati wa asubuhi na wakati wa jioni. Hivyo ni sehemu hatari iwapo waya huo utaanguka au kutokea mlipuko unaoweza kusababishwa na hitirafu ya umeme. Nimechunguza na kugundua kuwa kuna nguzo inatoka upande huo unaoonekana kwenye picha inavuka kwenda upande mwingine tunaweza kuita Posta au blocks za UDSM kilichokuwa chuo cha Posta. Hivyo iwapo waya huo utaanguka basi ni dhahili kuwa utaangukia kwenye bodi ya gari litakolokuwepo hapo chini au mtu yoyote ataye kuwa anapita hapo. Nguzo ninazozizungumzia mimi si hizo za chuma zinazo onekana. Ni zile za kawaida za miti.Tahadhari kabla ya hatari. Wahusika fuatilieni hilo au kama kuna mtu anaweza wafikishia taarifa hiyo nalo ni jambo jema.
 
Back
Top Bottom