MNYOO JOGOO
Senior Member
- Apr 2, 2012
- 195
- 94
Tukiwa tumeshuhudia kumalizika kwa chaguzi za udiwani katika mikoa mbalimbali nadhani sasa ni wakati wa chama tawala kukaa na kutafakari wapi imekosea na wapi ijirekebishe ili dhahama hizi zisitokee siku zijazo. Mhimu iangalie kama mapokezi ya vijana wanaojiita wapambanaji waliohama kutoka chadema na kujiunga CCM kwa publicity kubwa na hamasa huku mwenyekiti akijivunia vijana hawa kwa furaha kuliko hata mapokezi mfalme mswati alipokuja kufungua maonyesho ya 77 KAMA kweli jukumu walilopewa wamelitimiza kadri ya matarajio ya muongozo wa chama.
Sitaki nizungumzie jinsi vijana wazuri- CCM walivyopokwa majukumu na kukabidhiwa mtoto wa kambo, huku tukitarajia kuvushwa katika dhoruba kubwa hili la kisiasa ambalo upinzani hususani chadema wameonekana kujidhatiti. Umoja wa vijana walibaki wakisoma magaziti ya uhuru wakati mwingine wakisali mioyoni mwao kuombea mambo yaende ndivyo sivyo ilimradi nyoyo zao zisuuzike kwani walijihisi kutengwa kwani majukumu ambayo walidhani ni haki yao kuyafanya sasa yalifanywa na wa watoto wa kambo.
Rafiki yangu aliniuliza hawa ni kina nani hata wapewe kipaumbele namna hii? Nikamuambia muulize mwenyekiti!
Makosa haya yasijirudia katika chaguzi zijazo - kwani kuwa na mtaji wa vijana ambao badala ya kuuzasera nzuri ya chama wanakuwa na mashambulizi personal kwa mpinzani as if bado wanamapenzi na chama icho ila ndoto zao zilikatishwa tu.