Yap, only in TZ, only in bongo Mkuu.
Hii issue ina solution mbili
Kwamba liwalo na liwe, fisadi ni fisadi, lazima sheria ichukue mkondo wake.
Ili legal system yetu isiwe kichekesho na kulinda credibility yetu [ kama imebaki ] yeyote yule aliyekwapua mali ya umma lazima afikishwe mbele
ya sheria. Bila kujali ni mwarabu, muhindi, mzungu au mbantu.
Pili ni Kwamba hii issue ni too sensitive, na hivyo "wazee wa busara" wakae na
kuwapatanisha watu hawa, papa na nyangumi. Wapatanishwe na mambo
yaishe.
Ni wasiwasi wangu kwamba solution ya pili ndiyo itafuatwa. Watapatanishwa na kila mtu atachukua hamsini zake na ufisadi kuendelea kama kawaida. Hii itakuwa kama kufunika moshi huku moto unawaka ndani.