With a light touch - only in Tz !!

Mag3

Platinum Member
May 31, 2008
13,063
22,755
Listi ya mafisadi ilikuwa bado mbichi na serikali ilikuwa bado inatafakari ifanye nini, ikaingia Richmond. Serikali ikachanganyikiwa kwa kuanza kujitokeza kwa dalili za wazi za wananchi kukosa imani na serikali walioiweka wenyewe madarakani. Wakati serikali haijakaa sawa EPA na watoto wake wakawa wanabisha hodi huku JF ikitema cheche kwa data za uhakika kama kawaida. Hofu kuu ikatanda ndani ya CCM na serikali yake na hoja kuu ikawa - hapa tusipocheza kama Pele tumekwisha.

Mbinu zikasukwa kwa mtindo wa zimamoto na hatua ya kwanza ikawa ni kuisafisha Richmond kupitia TAKUKURU. Wakati wanatambua kuwa Tanzania ya leo ni tofauti na ya juzi, maji yakawa yameshamwagika na kitendo hicho kikawa kama vile wamemwaga petroli kwenye moto. Haraka haraka Bunge likaunda tume kwa lengo la kuinusuru serikali. Vibangusilo vikapatikana lakini kwa vile moto ulikuwa unazidi kuwa mkali, ikaamuliwa bangusilo mkuu naye lazima aunganishwe - naye akakubali japo shingo upande.

Badala ya hatua hizi kupoza hasira za wananchi ndio mambo yakazidi kuwa mambo na hatari ya kuumbuana ikawa inapiga hodi. Haraka haraka mweka hazina mkuu naye akatoswa na ikaundwa timu ya wataalamu kufuta nyayo za wahusika na kuhakikisha hakuna nyaraka zote zenye ushahidi zimebaki sehemu husika kwa kile kilichoitwa uchunguzi wa kitaalam. Na sheria ya nyaraka za siri ikaanza kupigiwa kelele ku"preempt" kutolewa kwa nyaraka zaidi - luckily it was too late

Baada ya kujiridhisha kuwa hakuna tena ushahidi zaidi wa kuweza kuwatia hatiani mhusika/wahusika wakuu, mbinu ikasukwa ya kuwafikisha mahakamani waliotupiwa makombo na kuwaacha waliokaa meza kuu wakitanua. Lakini pamoja na hatua zote hizi, kiu ya wazalendo wanaolilia haki haikuweza kuzimwa. Mpiganaji moja akajitokeza live kufunua vizibo vya maji machafu - La haula, taharuki wakajitokeza maruga ruga wakataka kufunika kombe mwanaharamu apite - kumbe la kuvunda halina ubani!!

My take: Ni wapi ulimwenguni ambapo soo kama hii ya kisanii ingewezekana isipokuwa hapa bongo tu. Hivi sasa mafisadi watajitokeza na kuongea kwa kujiamini kuwa wako salama - but could they be in for a rude awakening. Heko wazalendo wote waliouona huu mchezo tokea mapema na wakafanya kile ambacho mwananchi yeyote mwenye uchungu na taifa lake aweza kukifanya - nawapa pongezi nyingi. Nimejaribu kuifupisha hii tetesi kwa sababu bado sina uhakika wake - On the other hand I really hope it is not true.
 
Yap, only in TZ, only in bongo Mkuu.
Hii issue ina solution mbili
Kwamba liwalo na liwe, fisadi ni fisadi, lazima sheria ichukue mkondo wake.
Ili legal system yetu isiwe kichekesho na kulinda credibility yetu [ kama imebaki ] yeyote yule aliyekwapua mali ya umma lazima afikishwe mbele ya sheria. Bila kujali ni mwarabu, muhindi, mzungu au mbantu.
Pili ni Kwamba hii issue ni too sensitive, na hivyo "wazee wa busara" wakae na kuwapatanisha watu hawa, papa na nyangumi. Wapatanishwe na mambo yaishe.
Ni wasiwasi wangu kwamba solution ya pili ndiyo itafuatwa. Watapatanishwa na kila mtu atachukua hamsini zake na ufisadi kuendelea kama kawaida. Hii itakuwa kama kufunika moshi huku moto unawaka ndani.
 
Last edited:
Yap, only in TZ, only in bongo Mkuu.
Hii issue ina solution mbili
Kwamba liwalo na liwe, fisadi ni fisadi, lazima sheria ichukue mkondo wake.
Ili legal system yetu isiwe kichekesho na kulinda credibility yetu [ kama imebaki ] yeyote yule aliyekwapua mali ya umma lazima afikishwe mbele
ya sheria. Bila kujali ni mwarabu, muhindi, mzungu au mbantu.
Pili ni Kwamba hii issue ni too sensitive, na hivyo "wazee wa busara" wakae na
kuwapatanisha watu hawa, papa na nyangumi. Wapatanishwe na mambo
yaishe.
Ni wasiwasi wangu kwamba solution ya pili ndiyo itafuatwa. Watapatanishwa na kila mtu atachukua hamsini zake na ufisadi kuendelea kama kawaida. Hii itakuwa kama kufunika moshi huku moto unawaka ndani.

Ninalojiuliza ni hili - je yawezekana kuwa timu iliyojumuisha mkuu wa polisi, mkuu wa sheria na mkuu wa kupiga vita rushwa, kazi kubwa waliyoifanya ni kufuta nyayo za mafisadi ? Kwamba hii timu ilijikita zaidi katika kunyofoa na kuharibu ushahidi ili kulinda wakubwa?
 
If we are talking about hypothetical situations we might as well discuss other radical ideas such as the anti-gravity engine..lol
 
Serikali itawachukuliaje hatua Mwanyika na Hosea[ kama ilivyopendekezwa na tume ya bunge] iwapo hao hao wametumika kufuta ushahidi ambao ungewatia hatiani mafisadi papa wa Kagoda?
 
Serikali itawachukuliaje hatua Mwanyika na Hosea[ kama ilivyopendekezwa na tume ya bunge] iwapo hao hao wametumika kufuta ushahidi ambao ungewatia hatiani mafisadi papa wa Kagoda?

Swali la pili ninalojiuliza - Yawezekanaje kwa jina la mfanya biashara mkubwa kama RA aliyewapa ajira si chini ya watanzania 6000 kukosekana kwenye taasisi zote husika za serkali ? Tume ya Mwanyika, Mwema na Hosea ilichunguza nini karibu mwaka mzima na kutumia mamilioni kama hata jina la mmiliki wa KAGODA hawakuweza kulibaini ?
 
Jamani, Hivi Lowassa kajichimbia wapi? simsikii tena, kulikoni!

Nasikia kaonekana Marekani ,sasa sijui anamsaka Balali au anatafuta timu ya Basketball ajiunge ,labda walioko huko watujulishe ,kuna mtu aliandika hapa kuwa Balali ameanza kuonekana japo kwa mbali.
 
Back
Top Bottom