Wingi wa wabunge sio Muhimu bali michango | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wingi wa wabunge sio Muhimu bali michango

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Njowepo, Oct 28, 2010.

 1. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Watanzania wameaswa kupeleka bungeni wabunge wenye uwezo wa kutoa michango katika maendeleo badala ya kuchagua kwa nia ya kujaza idadi ya wabunge wanaohitajika.
  Wito huo umetolewa jana jijini Dar es Salaam na Musa Billengeya, Mratibu wa mpango wa Ondoa Umaskini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), alipokuwa akiwasilisha mada iliyohusu ``Historia na mazingira ya kisiasa katika chaguzi za Tanzania`` wakati wa semina iliyowakutanisha waangalizi wa uchaguzi kutoka Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (Sadc).
  Billengeya alitoa wito huo kama jibu la swali aliloulizwa na mmoja wa waangalizi wa uchaguzi, aliyetaka kujua kama wanawake wanaoingia bungeni kupitia viti maalumu wana michango ya maana kwa maendeleo ya nchi.
  “Katika suala hili la michango ya wabunge wetu, tusiwaangalie wanawake tu, lakini tuangalie wabunge wote kama wana michango yenye tija bungeni.Tuna wabunge ambao toka wameingia bungeni hawajawahi kuuliza swali, wala la nyongeza, achilia mbali kuchangia mijadala bungeni,” alisema.
  Billengeya alisema kwamba pamoja na kutochangia kitu chochote, inapokuja kwenye kusaini posho na kupokea mishahara huwa wa kwanza kuchukua na mbaya zaidi hata kwenye majimbo yao wanakuwa hawana mchango wa maana wanaoutoa.
  Aliwashauri wananchi kuhakikisha kwamba suala la idadi ya wanawake kufikia nusu ya wabunge wote katika uchaguzi huu, isiwe ndio mwongozo ila walenge kupata wabunge watakaochangia kwenye ustawi wao. Kuhusu kutoa elimu ya uraia kwa wananchi ili waelewe haki zao, Billengeya alishauri wadau wote wanaohusika, jumuia za kijamii, serikali na wahisani waanze mapema kutoa elimu hii.
  “Elimu ya uraia kutolewa miezi mitano kabla ya uchaguzi haiwezi kuleta tija inayohitajika. Ni muhimu elimu ikatolewa mapema na kwa muda mrefu ili wananchi waelimike na waweze kuchagua viongozi bora,” alisema.
  Alisisitiza kuwa wahisani ni muhimu wakaliona hili kwa kuwa wao ndio wanaotoa fedha za kuendesha programu mbalimbali za elimu ya uraia katika kuwajengea wananchi uwezo wa kufanya maamuzi yenye tija.
  Awali, Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, aliwaambia waangalizi hao kwamba kwa sasa Tanzania ina sheria inayokataza vitendo vya rushwa kwenye uchaguzi, lakini akasema ili kuitekeleza kwa ufanisi zinahitajika nguvu za pamoja kati ya Serikali na wananchi.
  Alisema mategemeo ya kutungwa kwa sheria hiyo ni kuifanya Tanzania iwe nchi isiyokuwa na rushwa kabisa kwenye uchaguzi.
  Kwa upande wake, kiongozi wa waangalizi hao, Shaboyo Motsamai, alisema nia ya Sadc ni kuona nchi zinazounda Jumuiya hiyo zinaendelea kuwa na amani pamoja na uongozi wa kidemokrasia kwa manufaa ya ustawi wa kanda hiyo.
  Alisema watazingatia sheria na kanuni za uchaguzi katika kuendesha shughuli zao hapa nchini wala hawatakipendelea chama chochote na kwamba watatoa ripoti ya kile watakachokiona.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Mimi napingana kabisa na huyu msomi. CCM wakekuwa wakipitisha miswaada mingi ya kishetani bungeni kwasababu ya wingi wao. Hiyo ni dark side demokrasia, linapokuja suala la kura kama wengi ni wajinga hao hao ndiyo wataamua musitakabari wa nchi.

  Na kwama Bunge letu ambalo masilahi ya chama ni juu ya nchi wingi wa wabunge ni muhimu sana.
   
Loading...