Kama bendera hizo zinapepea kwenye maduka ya wafanyibiashara wa huko, itakuwa wanatekeleza 'maelekezo' ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Fredrick Sumaye, kuwa ukipeperusha bendera ya CCM kwenye biashara yako, ni kama vile umeweka 'hirizi' ya biashara ambapo utavuta wateja wengi sana!
Lakini alichokuwa anamaanisha kiuhalisia ni kuwa kwa sababu wao ni chama dola. kwa hiyo 'wamewaelekeza' wakusanyaji mapato kuwa, wakifika kwenye biashara ambako bendera za chama tawala zinapepea, basi 'wawamezee' kwa kuwa hao ni wenzao na wafadhili wao wakubwa ambao ndio wanaokipiga 'tafu' chama chao, hasa hasa wakati wanapoingia kwenye kinyang"anyiro cha chaguzi mbalambali, wanapopambana na vyama vya upinzani!