win win situation fot TZ

Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
6,408
8,904
Je sisi kama Watanzania tunapaswa kumshukuru mkoloni (Mjerumani) kwa nchi yetu?
Baada ya kutafakari sana nimeona kwamba tuna kila sababu ya kumshukuru mkoloni au yeyote aliyechora mipaka yetu kwani tumependelewa sana, hakuna nchi yenye sifa kama yetu Afrika, tumezungukwa na maziwa makuu 3 na yote hayo tunamiliki zaidi ya 40%, tuna ufukwe wa Bahari ~km 1000, tuna visiwa kama mafia, tuna mito mirefu ambayo baadhi imo ndani ya mipaka yetu kabisa n.k sasa hoja ni kwamba yule aliyechora hii mipaka angeweza kuchora vingine na kukosa sehemu kubwa ya hivyo vitu!

Sasa Je ni sawa labda kubadili mtazamo na badala ya kulalamikia ukoloni na kuanza kusifu kwani sisi kwetu ni "win win Situation" ukilinganisha na nchi nyingi kama sio zote za kiafrika ukoloni umeleta madhara sana kwao?
 
Mjerumanai alikuwa na akili sana. Yeye ndiye aliyeitisha mkutano wa Berlin 1884 halafu akajichagulia vilivyo vizuri....Deutsche Ostafrika (Tanganyika) na Namibia...akaacha mifupa ndiyo hizo MALAWI ZA LEO
 
Je, nini maoni yako unafikiri ni sawa kwetu kuanza kuona kwamba ukoloni kwetu umetunufaisha?
 
Mbona maji ya mto Nile kutoka ziwa Victoria yanazengwe kubwa tu,
Sasa ziwa Nyasa tena zengwe hilo, Tushukuru au tuamke kutetea kilicho chetu?
 
Je sisi kama Watanzania tunapaswa kumshukuru mkoloni (Mjerumani) kwa nchi yetu?
Baada ya kutafakari sana nimeona kwamba tuna kila sababu ya kumshukuru mkoloni au yeyote aliyechora mipaka yetu kwani tumependelewa sana, hakuna nchi yenye sifa kama yetu Afrika, tumezungukwa na maziwa makuu 3 na yote hayo tunamiliki zaidi ya 40%, tuna ufukwe wa Bahari ~km 1000, tuna visiwa kama mafia, tuna mito mirefu ambayo baadhi imo ndani ya mipaka yetu kabisa n.k sasa hoja ni kwamba yule aliyechora hii mipaka angeweza kuchora vingine na kukosa sehemu kubwa ya hivyo vitu!

Sasa Je ni sawa labda kubadili mtazamo na badala ya kulalamikia ukoloni na kuanza kusifu kwani sisi kwetu ni "win win Situation" ukilinganisha na nchi nyingi kama sio zote za kiafrika ukoloni umeleta madhara sana kwao?

Tusipokuwa makini, hii issue ya Lake Nyasa yaweza kuwa 'Win Lose conflict of Agreement'.
 
Back
Top Bottom