Wimbo Wa escrow

Wimbo Wa escrow

don edy

Member
Joined
Nov 15, 2014
Posts
24
Reaction score
6
RAIS KUHUTUBIA TAIFA

IJUMAA TAREHE 19/12/2014!



MDAU HUYU👇👇, KAAMUA KUITUNGIA SHAIRI KABISAAA SIKU HIYO MAALUMU!
😄😄😄😄😄😄😄👍👍👍
👇👇👇👇👇👇👇👇👇👇


NA IFIKE-IJUMAA!

(1) Na ifike ijumaa, twaisubiri kwa hamu,Hatutaki kuzubaa, siku ya mashamushamu,Kusuka ama kunyoa, kwao wezi wa kalamu,Na ifike ijumaa, tuone hatima yao


(2.)Mmoja kakata kamba, kakimbia machinjio,
Imekuwa ni kasumba, wakikosa kimbilio,
Wengine wayumbayumba, kama siku ya gulio,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao.


(3)Ijumaa sio mbali, twangojea uamuzi,
Naona moshi kwa mbali,wafuka bila ajizi,
Walishaonja asali, mzinga hawauwezi,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao!


(4)Shoka limo shinani, kukata lipo tayari,Limeanza mitaani, kutanguliza habari,Laendelea mwakani, wakizidisha jeuri,Na ifike ijumaa, tuone hatima yao!


(5)Majizi yote pembeni, twaja mbio tupisheni,
Utani weka pembeni, ofisi zetu pisheni,
Fedha zetu rudisheni, vifungo ni haki yenu,
Na ifike ijumaa, tuone hatima yao!
 
Je ni kweli mabadiliko yatafanywa kwenye baraza la mawaziri?
 
Wakikamatwa Wezi Hao Na Kuwekwa Ndani Ntakunya Hadharani Kuanzia Manzese Hadi Ubungo
 
tupe tone tuimbe au ni utenzi
 
Ninaomba Mungu rais awe na moyo kama wa farao ili 2015 litimie andiko la kuizika ccm
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom