Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,345
[JFMP3]https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=177707&d=1408090155[/JFMP3]
SHUSHA HAPA: View attachment Vuma - Vitali Maembe.mp3Mashairi:-
Vuma
We mama mkaa ndanii, Toka nje usikiee,
Kutwa we kila siku ndanii, Toka basi usikiee.
kuna habari ina vumaa
Vuma x6
Na wee kaka Ughaibuni, Rudi Afrika usikie,
Wewe miaka yote mbali eeh, Rudi basi usikiee,
Kuna habari ina vuma
Vuma x6
Huko unguja mawee, Huko unguja maweee,
Kuna mtu kasimama, Kwenye kona ya Jahazi,
Anahoji uhalali, Uhalali wa Muungano.
Na mwingine kasimama, juu ya kidau chake
Analilia nchi yake, analilia Zanzibari eeh
Huko bara nakoo, kunamtu kasimama
Juu ya kaburi lake, analilia roho yake
Analilia Tanganyika eeh, Vuma vuma vuma
Vuma x6
Safu safu wanapita, wamejaa kwenye mitaa,
Na mabango wameshika, Wanalilia gesi yao,
Wanalili nchi yao wanalilia jina lao
Na wengine wanajipanga waje wadai mlima wao,
Watadai mito yao, Watadai migodi yao,
Watadai mbuga zao, Watawaua na wenzao
Kumbe imekwisha, Kumbe imetoweka amani eeh
Kumbe imepita, Kumbe haina hodi vita
kumbe imefika
Kumbe si demokrasia, kumbe ni demoghasia
Kumbe si democracy, kumbe ni democrazy
‘demonstration of craziness'
Viongozi wanajivunia kuwa watanzania
Wananchi wanavumilia kuwa watanzania
Nchi imetiwa giizaa, Macho yana kiu ya nuuruu
Kumbe imekwisha, Kumbe imetoweka amani eeh
Kumbe imepita, Kumbe haina hodi vita
kumbe imefika
We mama mkaa ndani
Toka nje usikie, kutwa we kila siku ndani eeh
Toka basi usikie.
Na wee kaka ughaibuni, Rudi Afrika usikie,
Wewe miaka yote mbali eeh
Rudi basi usikie, kuna habari ina vuma
Vuma x6