Wimbi la wazee vikongwe na ajira ya ulinzi

Wimbi la wazee vikongwe na ajira ya ulinzi

yutu

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2013
Posts
1,778
Reaction score
1,223
Inasikitisha sana kuona sehemu nyingi sana za biashara na public services kama hospital, market areas, hotel etc zinakuwa na walinzi wazee sana (vikongwe) kuanzia umri wa miaka 70 mpaka 80, mazingira na vitendea kazi havijitoshelezi kumfanya afanye kazi impasavyo.

Wengi wamekuwa kama 'boshen' tu. Ataripoti kazini saa 2 ataondoka kwenda kunywa gongo, ulanzi au mchujo kurudi saa 6 au 7.

Silaha aliyokuwa ni manati au panga. Je, mwizi au jambazi aliedhamiria kufanya uhalifu atashindishwa kumdhibiti mlinzi wa aina hii kweli?

Mlinzi anaefanya kazi katika mazingira kama haya 'amekunywa' siku ipite akipata mchongo wa kuihujumu kazi yake, atashindwa kushawishika kweli?

Wastaafu wa majeshi yetu ya ulinzi na usalama wameusika sana kwenye issue hizi kama si kufungua kampuni uchwara za ulinzi basi ni kuajiri au kutafuta ajira kwa kigezo cha wao kuwa na uzoefu wa masuala ya ulinzi na usalama matokeo yake matatizo yanapotokea sehemu husika wao huwa mbali kabisa na hao waliowaajiri mwisho wake hupelekea kufungwa, kudhurika au kupoteza maisha kabisa.

Cha kujiuliza ni kuwa hivi hawa vikongwe walipokuwa kwenye system 'walikula ujana' pasi kujua kesho inajengwa na leo?

Hawa waajiri hawajawaona watu wenye sifa stahiki mpaka wawaajiri hawa vikongwe?

*kula sana ujana ukumbe fainali uzeeni*
 
Acha maisha yawapige tu unakuta ujana wote kaumalizia kwenye viuno vya kina Dada.....
 
Sababu ni cheap labour. Analinda usiku mzima kwa mwezi mshahara 50,000.

Vijana hawataki
 
Na wengi wao wanatumia nguvu za kishirikina ndio maana wanapewa ulinzi na wanaowafahau usifikiri wapo tuu wamejikoki vya kutosha hata mlizi mwenye k47 haoni ndani
 
Acha maisha yawapige tu unakuta ujana wote kaumalizia kwenye viuno vya kina Dada.....

Unasahau kuwa
Wenngine ni wale walidhurumiwa na serikali yako?
Wengine ni wale walikupigania wakati wa vita ya Uganda na Tanzania
Wengine ni wale walisamehe shule ili wenzao katika familia waweze kusoma na kwa mapenzi ya Mungu hawakuweza kuendelea kuishi,
Usihukumu usije ukahukumiwa
 
kumbe wengi ni washirikina? mhh halafu inawezekana, kuna Jirani yetu ana miaka 75 analinda duka la muhindi usiku namshangaaga sana maana siku nyingine anakua kachoka saana lakini anakwenda kazini tena usiku ni balaa
 
Na wengi wao wanatumia nguvu za kishirikina ndio maana wanapewa ulinzi na wanaowafahau usifikiri wapo tuu wamejikoki vya kutosha hata mlizi mwenye k47 haoni ndani

Nikweli kabisa wengi wao wanatumia ushirikina, yaani babu moja tena ana rungu analinda store yenye mali za 300 Mil.
 
Unasahau kuwa
Wenngine ni wale walidhurumiwa na serikali yako?
Wengine ni wale walikupigania wakati wa vita ya Uganda na Tanzania
Wengine ni wale walisamehe shule ili wenzao katika familia waweze kusoma na kwa mapenzi ya Mungu hawakuweza kuendelea kuishi,
Usihukumu usije ukahukumiwa

Nani kahukumu?

Kusema reality n kuhukumu?
 
Naumia sana kumuona mzee anaangaika kutafuta riziki. Its not fair at all. Hawa ndio waliweka misingi yataifa na taifa bila kubagua mzee yeyote ina wajibu wa kuwatunza kwa kuwapa huduma za kijamii social welfare. Watoto na akina mama wasiojiweza nao wanaangukia kundi hili la wazee. Inaniuma sana nchi yetu inaendeshwa kimungu mungu tu. Ustawi wa jamii unafanya nini????
 
vijana ni waoga wakiona vibaka wanatoka baru.
 
Back
Top Bottom