Wimbi la viongozi wa dini kubaka, dini zao zifutiwe usajili

Sir robby

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
2,404
4,053
Hakika inashangaza sana Kuona Wimbi la Ubakaji wa viongozi wa dini Limekuwa kubwa kwa sasa. Je kama Mchungaji au Shehe anaweza kubaka mtoto wake, je anawabaka Watoto wangapi wa Waumini Wake?

Nadhani ni Muda sahihi serikali kufanya Uchunguzi kwa Madhehebu yote Kuona kama yanakidhi vigezo kwa viongozi wake na kama hawakudhi basi Serikali Iyafungie na kuyafutia usajili.

Inashangaza Mtu anaibuka na Kujenga kijumba cha Mabati Chakavu na Kutundika msalaba kisha Yeye na Mke ndio Viongozi wa Kanisa hata Elimu ya Dini hawakupitia kwenye Chuo chochote na Serikali inatoa usajili Matokeo yake ni haya.

1665602162377.jpg
 
Hawawezi kugusa huko maana ni hatari, ujasiri wa kupambana na mafisadi na wanajisi wa kidini wanao viongoz wachache sana, labda kagame, ila hawa viongoz wetu hawawezi.

Hao wanaowapa mikopo na masharti ya kishenzi ndio hao hao wamiliki wa makanisa na dini zote, isitoshe dini hizi wanazitumia kama njia ya intelegensia ya kupata siri zenu za nchi.

La muhimu hapo ni raia sasa kuachana na haya magenge ya kidini, mwanaume kamili hawezi kuishi bila mwanamke, unapomuwekea masharti ya kijinga ndio hapo anaanza kutenda matendo ya kishenzi kama hayo, isitoshei dini zao ktk sirini kufanya hayo machafu ni aina za Ibada ama matambiko kwa Miungu yao, eeh miungu, maana washika dini hamna elimu yoyote kiundani kuhusu Hao mnaowaabudu, aje Kiongozi mkubwa hapa wa Dini apinge hili.

Ngono, ushoga, umwagaji damu,ibada za Kuabudu Mizimu, Kucontroll serikali za mataifa, kutumia imagination za Miungu kama silaha za kuharibu akili, haya yote wanayafanya nyuma ya pazia hao jamaa zenu mnaowaamin na kuwatumikia eti maaskofu sjui wachungaji, hakuna uchungaji wowote zaid ya uhuni tu.

Amkeni jamn mnapotezewa muda huko
 
Wenye akili tushajua nn kinatafutwa.

Ktk maono inaonekana,

Kiongozi anaingia ktk nyumba za ibada ameshika kitabu Cha Sheria.

BAADAYE kiongozi huyo huyo atakuja kukabidhi jambo Fulani Kwa kanisa baada ya kushindwa plan ya kwanza.

Ameeeen.
 
Una uwezo wa kulifuta kanisa lile wewe ? linalokuchagulia mpaka Rais ?
 
Inashangaza Mtu anaibuka na Kujenga kijumba cha Mabati Chakavu na Kutundika msalaba kisha Yeye na Mke ndio Viongozi wa Kanisa hata Elimu ya Dini hawakupitia kwenye Chuo chochote na Serikali inatoa usajili Matokeo yake ni haya.
Ndiyo maana Kagame ameyafuta haya makanisa-mtu na kuweka sheria vigezo na masharti makali ya kuanzisha kanisa.

Makanisa-mtu ni miradi kama miradi mingine
 
Hizo ni tuhuma mkuu tuache vyombo vya kutafsiri sheria vifanye kazi yake na kingine kubaka ni utashi wa Mtu binafsi sio kanisa au msikiti umemtuma kufanya hivyo
Waingereza wanasemaga Rumors is carried by haters spread by fools and accepted by idiots. !! Watu wabaya wakimzushia mtu jambo baya na kuanza kulitangaza kuanzia vijiwe vya kahawa , bodaboda, bajaji basi baada ya muda mfupi mji mzima utaenea huo uzushi ambao umetengezezwa tu !! Ndipo tulipofikia kama Taifa. !! Ni msiba mkubwa !
 
Hujazungumzia walimu wa madrasa wanaolawiti na BAKWATA kukaa kimya kama BAKWATA inastahili kuendelea na usajili?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom