Kwa uzoefu wangu wa ukondakta wa daladala....kazi ya ukonda ina changamoto nyingi sana ambazo zinahitaji uwe shupavu sana....na nilishawahi kufanya kazi na wanawake mlangoni lakini maumbile yao kibaolojia hayaendani na kazi....kwa mfano unaweza ukampitia mkaamshe gari anakwambia leo nipo kwenye siku zangu na tumbo linanisumbua...inabidi utafute mtu mwingine wa dharula....mara utasikia kashikwa na tumbo la chango..................yaani ni full majanga......kwa kifupi hii kazi wanawake haiwafai...........