Nimefanya utafiti mtaani na vyuo vikuu nimegundua kuwa kuna mabinti wengi wanabeba mimba kabla ya ndoa wengi ni mabinti wadogo sana, nikarudi nyuma kidogo ilikuwa ni vigumu kumkuta binti anabeba mimba kabla ya kuolewa lakini siku hizi imekuwa kawaida sana, matokeo yake tunatengeza kizazi cha hovyo na cha ajabu sana.
Maana asilimia kubwa wanaobebeshana mimba hawaoani hali inayopelekea ugumu katika malezi ya watoto hao, tatizo lingine lipo kwa wazazi maana ni kama wameshindwa malezi ya watoto wao hali inayopelekea kufanya mambo ya ajabu kama haya ya kuzaa kabla ya ndoa upo wapi ule msimamo wa wazazi katika malezi ya watoto, lakini vijana wengi wanafanya hivyo bila kujua madhara jambo hili.
Tujisahihishe maana malezi ya watoto yanahitaji pande mbili baba na mama wasichana msikubali kurubuniwa kirahisi na kukubali kubeba mimba kama mtu anakupenda mwambie aende kwenu taratibu zote zifuatwe ndoa ifungwe umzalie watoto ukiwa ndani ya ndoa hii ya kuzaa kabla ndoa inaharibu maisha yenu maana wengi mkizalishwa mnaachwa huku mkihangaika kulea watoto wenyewe.