Umuhimu wa ndoa imepungua sana kwa wote wanaume na wanawake. Tunachotafuta ndani ya ndoa kinapatikana bila ndoa. Ya nini kujifunga? Miaka mia ijayo ndoa zitakuwa historiaNafikiri ni kwa sababu leo watu hawajui ni nini hasa maana ya ndoa,walio wengi hasa wale vijana wa kileo wao huwaza ndoa ni starehe ya ngono tu au kupata unafuu wa maisha hawajui kuwa ndoa ina wigo mpana zaidi na inamaanisha uwajibikaji wa miaka yote ya mtu mpaka kifo,na kwa sababu hiyo mara mtu asiyejua nini maana halisi ya ndoa aingiapo ndani ya ndoa na kujua maana halisi ya ndoa ni tofauti na ile aliyoidhania hushindwa kuhimili na hapo ndipo talaka huanzia nadhani.
mashini, tulisha lizungumza hili sana kiasi watu wanaweza kuchoka kusoma tena comments!
Ila kwa kifupi, kwa mtazamo wangu, wengi wao huwa hawajafahamiana vizuri (wale wanaokutana kwa muda mfupi) au hawajajiandaa kuishi maisha ya ndoa kisaikolojia (wamelazimishwa na familia, kupeana mimba, mazingira nk) au kuiga (kwa sababu age mate wake wote wameoa/kuolewa) au kwa nia ya kupata mtoto tu au kwa nia ya kupata mali tu toka kwa mpenzi wake, kutokujuana tabia halisi mapema, kudanganyana nyakati za uchumba na ukweli kujulikana baadaye nk.
Pia udigital umetuponza
Watu wanaishi maisha fikirika inapofikia anaingia kwenye ndoa akikuta maisha si vile alivyofikiria b4 kinakua chanzo cha ndoa kuvunjika.
Watu wengi sana wanatamani kuishi maisha kama yale wayaonayo kwenye movie pasipo kujua kuwa yale ni maigizo tu sasa anapokuta uhalisia hauendani na fikra zake ndoa inakuwa ndoano.
hebu fikiri kijana anapoingia mwaka wa tatu chuo kikuu, anachokiwaza wakati huo juu ya maisha atakayoishi baada ya kuhitimu masomo yake ni tofauti na anachokikuta mtaani.
Wamefanya nini
Faida ya kuoana ni pamoja na kuunganisha familia za pande mbili za upande wa mwanaume na mwanamke; Hii ina maana kwamba mnaongeza wigo wa kusaidiana katika kazi na maisha kwa ujumla. aidha, ni aibu katika maisha kuingia katika talaka, bali ni hekima kujifunza namna ya kufanya ili uendelee kuwepo kwenye ndoa kwa amani, kama ndo hivi kwanini kuna wimbi kubwa sana la ndoa kuvunjika kwa sasa?
Hivi siku hizi ni nani anakaa kufundisha hawa walengwa maana halisi ya ndoa ni nini?
Mie nishauri tu kwa upande wa makanisa,ndoa ifanywe kama somo la muda wa kutosha,waandae mafundisho ya ndani zaidi na ikiwezekana kuwepo na mitihani kwa wale wanaojiandaa na ndoa na pia mafunzo haya yazingatie changamoto za sasa,mfano wafundishwe vipengele ama topics za kuvumiliana topic,kusamehe topic,kupata ama kukosa mtoto topic,kuheshimiana topic n.k siyo kama leo toka maandalizi hadi ndoa ni wiki2, kweli?
Nafikiri ni kwa sababu leo watu hawajui ni nini hasa maana ya ndoa,walio wengi hasa wale vijana wa kileo wao huwaza ndoa ni starehe ya ngono tu au kupata unafuu wa maisha hawajui kuwa ndoa ina wigo mpana zaidi na inamaanisha uwajibikaji wa miaka yote ya mtu mpaka kifo,na kwa sababu hiyo mara mtu asiyejua nini maana halisi ya ndoa aingiapo ndani ya ndoa na kujua maana halisi ya ndoa ni tofauti na ile aliyoidhania hushindwa kuhimili na hapo ndipo talaka huanzia nadhani.