Wimbi la jeshi kuwaunga mkono wananchi ni tishio kwa watawala

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,921
71,500
Limejitokeza wimbi la wanajeshi na polisi sehemu mbalimbali duniani kuunga mkono maandamano na harakati za wananchi kuwaondoa viongozi dhalimu, madikteta na mafedhuli.

Zamani ( nahata sasa) wengi walikuwa wanalindwa sana na vyombo hivyo na walidumu kwa sababu wananchi wakianzisha wana dhibitiwa kwa kipigo hata mauaji bila woga wala hofu.

Tumeshuhudia majeshi yakiunga mkono raia hadi kuondoa utawala bila kutumia nguvu kubwa na RAIA kubaki salama huko Misri, Algeria, Sudan, Zimbabwe na Jana huko Bolivia.

Sasa hivi viongozi madikteta au mafisadi ni suala tuu la kupata wa kuandaa maandamano na migomo bila woga wa KUCHAKAZWA KAMA MBWA KOKO kisha kulianzisha na kuungwa mkono na jeshi mradi sababu ziwe za msingi tuu.
Njia zile za zamani za mapinduzi ya kijeshi zimepitwa na wakati na hazikubaliki tena.
Poleni madikteta duniani!
Screenshot_20191112-092446.jpeg
 
Obote alijichanganya akamuweka mzalendo wa Afrika mwanamapinduzi wa ukweli Field marshall Iddi Amin Dadaa kuwa mkuu wa Majeshi, kilichotokea hapo ilibidi rafiki yake aingie front kumpigania ili arudi madarakani.

Siku moja "Danganyika" wajichanganye wakosee vetting wamuweke mtu asiyekubali mambo ya ajabu ajabu kuwa mkuu wa Majeshi hapo ndo watajua Jeshi halinaga rafiki, na wala Jeshi huwezi kulichukulia poa wala kujidai unalijua sana!

Wacha waendelee kuaccumulate makosa tu, hayo makosa ndo yatatumiwa kwenye tangazo maalum redioni na kwenye television kujustify sababu za hatua iliyochukuliwa!
 
Wanajeshi watz wameungana na wananchi kuitoa ccm madarakani. Na Lisu na Chadema wameshika dola kwa sasa.

Haya furahi sasa!
 
Mungu atufanyie wepesi
 
Huyo Rais morales aliingia madarakani akaanza mbwembwe hadi akajitapa kiboko ya mabeberu na staili yake ya uongozi vinafanana na vya huyu wa kwenu hili ni funzo kwa viongozi wanaojifanya bila wao hakuna anaeweza kuongoza.
 
Kwasisi bado maana hao wanajeshi na mapolisi kibao wana kadi za kijani,njaa kali,uoga na kujipendekeza kupitiliza.
 
Obote alijichanganya akamuweka mzalendo wa Afrika mwanamapinduzi wa ukweli Field marshall Iddi Amin Dadaa kuwa mkuu wa Majeshi, kilichotokea hapo ilibidi rafiki yake aingie front kumpigania ili arudi madarakani.

Siku moja "Danganyika" wajichanganye wakosee vetting wamuweke mtu asiyekubali mambo ya ajabu ajabu kuwa mkuu wa Majeshi hapo ndo watajua Jeshi halinaga rafiki, na wala Jeshi huwezi kulichukulia poa wala kujidai unalijua sana!

Wacha waendelee kuaccumulate makosa tu, hayo makosa ndo yatatumiwa kwenye tangazo maalum redioni na kwenye television kujustify sababu za hatua iliyochukuliwa!
Kwamba siku wajichanganye wampe msonjo silaha hahaa.
 
Wanajeshi watz wameungana na wananchi kuitoa ccm madarakani. Na Lisu na Chadema wameshika dola kwa sasa.

Haya furahi sasa!
Naona unmtabiria Lisu uhalisia. Ungelijua kuwa jambo la Lisu si la mzaha kihivyo, na kwamba katika tukio lile alikosekana tu wa kulianzisha vinginevyo leo jiwe angekuwa historia!!!
Umewahi kufikiria kwa nini ndege iliyompeleka Lisu iliruhusiwa kutua Dodoma bila figisu. Basi leo nikuambie kwamba wapangaji na watekelezaji wa mauaji ya Lisu walipoteana. Sasa unajua kwa nini walipoteana!!!?
 
Kwahiyo ilitua bila figisu, kwamba iliruhusiwa na wanajeshi wakishirikiana na wananchi?
 
Back
Top Bottom