William Ngeleja arejesha fedha za mgao wa Escrow kiasi cha Tsh Milioni 40.4

Dhambi ya usaliti haifi Hata siku moja Kuna siku itakutafuna.

William Mganga Ngeleja Kuna siku ataijutia dhambi ya usaliti.

Kwanini anarudisha pesa leo?

Anatoa ujumbe gani kwa wengine?

Anategemea tutamuelewaje?

Hapana usimlaani sana, ametusaidia kiaina kujua kama kweli serikali imeamua kulitumbua jipu la escrow kwani JK alituaminisha kwamba zile pesa sio za umma, sasa Ngeleja kazipeleka serikalini na wamezipokea ina maana ni za umma! Au ni utakatishaji? Muda utaongea
 
Usaliti haujawahi kumuacha mtu salama

Amewasaliti wahenga wenzie lama Rugemalira,mzee wa vijisent,Tibaijuka,yule askofu nk

Jamaa amejitenga na wahenga wenye uchu wa hela
 
Dhambi ya usaliti haifi Hata siku moja Kuna siku itakutafuna.

William Mganga Ngeleja Kuna siku ataijutia dhambi ya usaliti.

Kwanini anarudisha pesa leo?

Anatoa ujumbe gani kwa wengine?

Anategemea tutamuelewaje?
Kila mtu atabeba msalaba wake mbele za Mungu na kwa serikali.Kwa hiyo ni ujinga na sio sahihi kuangalia wengine wanafanya nini.Kama nafsi yake imemshuhudia kwamba kuchukua fedha zile haikuwa sahihi, basi alichofanya ni sahihi.
 
Mkuu hiyo nafsi yake imechelewa sana kumshuhudia. Ni nafsi ya aina yake hiyo iliyosubiri mpaka Ruge na Seth wakamatwe ndio imshuhudie. Hii nafsi yake inafanana sana na ya bwana yule aliyejiuzulu uenyekiti wa chama na akadai nafsi yake ilimsuta. Lakini nafsi hiyo hiyo ikamwambia tena arejee kwenye nafasi yake.
 
Kila mtu atabeba msalaba wake mbele za Mungu na kwa serikali.Kwa hiyo ni ujinga na sio sahihi kuangalia wengine wanafanya nini.Kama nafsi yake imemshuhudia kwamba kuchukua fedha zile haikuwa sahihi, basi alichofanya ni sahihi.
Amejua leo kuwa sio sahihi na kelele zote zile.....kuoa ulioa wewe halafu unakuja kutuambia hujui kama ulitakiwa kuoa! Unatoa talaka
 
Back
Top Bottom