Wilfred Lwakatare: Mrejesho kutoka mahabusu Segerea

lovey62

Senior Member
Apr 13, 2013
132
111
Salaam wakuu,

Mheshimiwa Kamanda W. Lwakatare aka PRISON GRADUATE ametoa makala yake ya kwanza iitwayo "MREJESHO KUTOKA MAHABUSU"

 
Kamanda, pole sana,hii ni moja ya shule ambayo mwanasiasa mahiri sharti akutane nayo katika maisha ya siasa zake katika kupigania haki. Nimesoma makala yako,imenipa simanzi lakini pia imenipa courage kwamba umepanua wigo wako wa kuifaham jamii,serikali na vyombo vya dola. Tumia elimu uliyoipata huko kuielimisha jamii. Waeleze watanzania hila na uzandiki uliotendewa na MWIGULU na CCM, TUAMBIE KWA UFASAHA LUDOVICK ilikuwaje akageuka kuwa YUDA WAKO...kukuharibia heshima yako kwa vihela vidogo na tena kwa kutumiwa na MWIGULU?...hata hivo,nakukaribisha katika vita ya ukombozi wa taifa hili kutoka kwa mkoloni mweusi, mnafiki na mhujumu wa uchumi na maisha yetu...
 
This is beautiful!

Wafungwa, mahabusu, baadhi ya watumishi wa gerezani, mapolisi na wengineo wanatoa salamu nyingi sana. Wengi wanaipongeza kazi inayofanywa na CHADEMA ndani na nje ya bunge. Wanasema karibu wote ni CHADEMA japo wengi hawana kadi. Ili upokelewe vyema gerezani lazima uwe ‘vidole viwili’ ukijitia ‘ukada’ utalijua gereza. Wanasema kamwe wabunge wa CHADEMA msitiwe woga na tambo za wabunge wa CCM ndani ya bunge kwa kujiona wako wengi wakifikiria huo wingi upo hata nje ya mjengo. Wanasema katika hilo ‘wamebugi meen!!’. Nje ya Bunge CHADEMA mna mashabiki na wafuasi nyomi!! Yaonekana kwa hivi sasa Bunge ni uwanja wa nyumbani anaoutumia CCM kimchezo na ninyi CHADEMA uwanja wenu uko huku uraiani kwa umma.

Issa Ponda ni kiumbe wa mwenyezi Mungu wa aina ya pekee. Kwa nchi za wenzetu zilizoendelea mtu mithiri ya Ponda si mtu wa kuchukulia mzaa kama ninaouona ukichezwa hapa kwetu. Ni mtu ambaye fikra zake, ubunifu alionao kichwani na katika vitendo, hulka zake, nasaha zake, ushawishi wake, ujengaji hoja zake, uchaji wa Mungu wake, uswalihina wake na vingine vingi ni watu wachache sana unaoweza kukutana nao wakiwa navyo vyote kwa mpigo.

Ponda tofauti na namna mfumo unavyomchukulia, ni mtu ambaye angetumika vyema kwa kusikilizwa sehemu kubwa ya mawazo yake na yakafanyiwa kazi ipasavyo, nina uhakika mambo mengi tunayoyaona yana mitafaruku ya kidini yasingelikuwepo.

Tatizo wakubwa wanamuangalia kwa taswira ya upande mmoja ya kumuona ‘mkorofi, mchochezi’. Sijui na ndio maana nauliza, hivi ni mamlaka gani ya juu na yenye kauli ndani ya nchi hii imewahi kukaa na Ponda kwa karibu katika misingi ya kuheshimiana kwa dhati na kusikilizana ili kujua ana mawazo na mitizamo gani kwa masuala mbalimbali yaliyolalamikiwa na baadhi ya waislamu walio wengi?

Nimeishi naye zaidi ya siku 60 selo moja kwa masaa 24 karibu kila siku na masaa mengi tukiwa wawili tu, mimi na yeye. Ni mdadisi wa kupenda kujua, na ukisha mwelewesha ni mwepesi wa kuelewa na kujenga fikra mpya. Hivyohivyo siyo mchoyo wa kuyabania maarifa aliyonayo na elimu kubwa ya kidini aliyobahatika kuipata.
 
Hii habari imeniliza machozi ni kweli watu kama Sheikh Ponda ni wakusikilizwa. Ila kumwita Prof nadhani Lwakatare umekwenda mbali.

Mkuu Masanilo, kamanda Rwakatare anajadili upande mzuri wa Ponda; upande ambao tumekuwa hatuoneshwi. Ukijenga urafiki na mtu huwa rahisi kumsemea mema mengi sana--pengine hata kupitiliza uhalisia wake, yote yakitokana na chemchemi ya upendo kwa huyo mtu. Mi naomba tulipokee hili.
 
Binafsi namfahamu sana Rwakatare, ni kiongozi wangu wa mkoa nami nikiwa kiongozi wilaya jirani. Kusema kweli sikuwahi kujua kama na uwezo wa kuandika kwa hisia kiasi hiki. Ameandika mambo yanayoweza kujenga chama chetu kwa mtazamo mpya kabisa. Asante CCM kwa kumpeleka kamanda katika retreat ya kipekee, amepata muda wa kufikiria kwa faida ya chama. Mungu akuongezee muda wa kuishi kamanda!

Tuna kazi kubwa ya kuimarisha chama mkoani kwetu, tunahitaji kuikomboa Kagera kuliko hata Tanzania! Tunakuandalia mapokezi yatakayoacha historia hata kiama. Njoo kamanda nadhani tunahitaji kujifungia sehemu tutafakari pamoja na ujumbe huu muhimu na mengine zaidi utakayotuasa ndani.

Karibu PRISON GRADUATE!
 
Kamanda umeongea Mambo Makubwa na ya kuogofya.Kwa ujumla umenitoa Machozi.Swala la Ponda limenisisimua zaidi.Nilikuwa namchukulia Ponda kama Miongoni mwa Watu hatari zaidi kwa Taifa kumbe sio.Tatizo ninaloliona ni Ukosefu wa Uongozi wenye Uwezo wa kusikiliza Hoja za Wananchi wake na Kuzitolea Ufafanuzi.Tumeachwa tufarakane kwa Mambo ya Hovyo kabisa.Siku zote Uongozi wa kununua huua Taifa.
 
Pole sana Lwaka. Nimejifunza mengi kutoka kwenye nakala yako hasa swala la watoto magerezani kweli ili tulipe kipaumbele maana watoto ndio Taifa la kesho. Ni lazima kama taifa tuwe na mipango ya jinsi ya kuwasaidia watoto wa magerezani.. Laiti kama Viongozi wetu wangekuwa wanavipaumbele basi hiki kingekuwa kipaumbele kimoja wapo hasa kwenye bejeti zetu mbali mbali kuliko bajeti za majeneza.

Swala la Ponda nalo nimejifunza kuwa si kweli Ponda ni mbaya vile ila ndio hizo propogada tulizozoea maana ukimsiliza Ponda katika Negativ way utapata ujumbe tofauti kama ukimsiliza in the positiv way.. Nilifikiri kuwa Ponda hawezi hata kukaa chumba kimoja ya mkristo ...
 
Pole sana Lwakatare, Makala yako nimeisoma kwa makini mno na imenisikitisha sana.
Karibu sana Uraiani.
 
I don't even know what to say to you Kamanda. It is a well researched summary, more to come in your coming book. Bravooo. Halafu wanasema CHADEMA hamna vichwa.. hawajajipanga. Kwa nguvu na mpangilio uliopo CHADEMA we are very capable kuongoza nchi 2015.

Kamanda Mungu akujalie afya ya mwili na roho malengo yako na yetu yatimie. People's ......
 
Madaraka ni mazuri na yana mambo yake,viongozi wengi wa kiafrika wamefanya maovu mengi sana wakati wa utawala wao,hii ni kwa sababu katiba na mifumo wanayofanyia kazi inawapa mamlaka makubwa sana za kimaamuzi bila kuhojiwa na mtu au taasisi yoyote ile,hali hii inawafanya kuwa waoga sana katika kuachia madaraka kwa watu wengine na hasa vyama vingine ambavyo vinaonekana kuwa havitakuwa tayari kufukia maovu ambayo wameyatenda wakati wakiwa madarakani.
Kiongozi gani wa CCM anapenda kuona anapelekwa jela kama Rais wa zamani wa Zambia Mh. Banda anavyopelekwa jela na Rais wa sasa Mh Satta?Hivyo basi CHADEMA lazima mjue kuwa sera zenu na msimamo wenu dhidi ya ulinzi wa rasilimali za nchi hii ni tishio kwa maisha ya baadae kwa viongozi wa sasa wa CCM ambao kama watakuja kubainika kuwa kuna makosa ambayo wameyafanya wakati wa utawala watakuwa kwenye wakti mgumu na nafikiri wengi wao wanliona hili na ndio maana wanajitahidi kulinda madaraka yao hata kwa kuuwa,kutoa watu kucha,meno na mengineyo.Kwa mantiki hiyo CCM kuachia madaraka sio kitu cha urahisi matukio kama haya ya kina Lwekatare lazima yatokee na yatakuja mengi zaidi ya haya,
Funzo tunaloplipata hapa ni kwamba SIASA sio mchezo,anaekubali kuingia katika siasa lazima akubaliane na Changamoto hizi,Maana pamoja na kuwasaidia wananchi siasa ni kazi kama kazi nyingine,ina changamoto zake amabazo ungeweza kukutana nazo kwenye eneo lako la kawaida la kazi,
Mungu awatie nguvu wana CHAEDMA msikate tamaa,kila safari ina hatua zake na matukio yake,si lazima kila mtu aifikie au aione siku ambayo mtaingia madarakani,kwani Mzee Bob Makani ameiona CHADEMA ikiingia madarakani?hajaiona lakini hakukata tamaa mpaka ameondoka na ameiacha CHADEMA inaendelea,Tunaamini "YUKO AROUND MAZEE" na anafurahia jinsi vijana wanavyochapa kazi.
Mungu amrehemu katika pumziko lake la Milele,Safari ni Moja na na sisi tunafuata,ila bora yeye Tunamkumbuka kwa alichokifanya,sijui mimi na wewe tunaoishia kuandika kwenye JF tu tutakumbukwa na nini?
TUWE SEHEMU YA MABADILIKO,TUWE SEHEMU YA KUKUMBUKWA KWA MAZURI KATIKA KUITETEA NCHI YETU!
Mungu IBARIKI CHADEMA,MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Samahani lkn, ingekuwa Ni kweli umepanga mpango huo ungetuwekea wazi hapa jamvini?
 
Inahuzunisha sana kwa kweli hasa hilo la watu kupewa kesi zisizo zao. Nani wa kuwasaidia watu hawa? Kumbuka leo ni kwa mwingine lakini kesho waweza kuwa ni wewe!! Pole Lwakatale kwa yaliyokufika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…