Wilfred Lwakatare: Mrejesho kutoka mahabusu Segerea

Pole sana Kamanda Lwaks tuko nyuma yako!kuhakikisha 2015 tunabadilisha upepo huu na ukombozi wa kweli upatikane!ni mapambano ambayo alieshika mpini hatakubali kirahisi,ila wenye nchi wakiamua inawezekana!tena kwa urahisi tu!nguvu ya sanduku la kura!pole sana ila usirudi nyuma na uwe makini sana!kuna kitu hujakiongelea ila najua sababu ya kesi iliyo mahakamani!hujaelezea ilikuwaje na mazingira yake ile CD na mshirika wako wa karibu!tunaona kuna kitu hujakimalizia!!
 
So painful! Mtatiro huijui CUF! Said Mwema na unafiki kwa college mate, kisa shemeji JK! Mwigulu mateso yote haya . . . . . . . . !
 
Last edited by a moderator:
Makala imejaa hekima nyingi na uhalisia wa asilimia kubwa i wish kila kiongozi, mwanachama, na mfuasi wa chadema angekuwa na maono kama haya na akayatekeleza bila unafiki basi wengi wangewaelewa chadema. Nakutakia maisha mema Lwakatale kwa maoni yako najua ni constructive kwa mustakabali wa taifa letu.
Ushauri: watu tusipende kuufukia ukweli japo unauma.
 
Pole sana,leo nimejua ni kwa nn CCM waliamua kukuchagua wewe kukuwekea kesi ya kutunga.Unaakili sana nimekumbuka hotuba yako bungeni wakati ukiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.Japo safari bado ngumu ila nina imani tutafika.
 
yote ya yote kamanda yana mwisho haya hasa ukizingatia tuna mess(lissu) lonardo(safari) van persie(mabele) bebeto(kibatala) pamoja na garrincha (nyaronyo kichere) panga magolikipa saba lazima utunguliwe
 
Aisee kamanda pole sana kwa yaliyokuta kweli siku 92 ulizokaa selo ni darasa tosha, lakini usichoke wala kuwatumikia watanzania ambao bado wanahitaji ukombozi wa fikra hasa huko vijijini na zaidi ya yote tunapaswa kujua kila kitu ni mpango wa mungu CCM siku zao zinahesabika baada ya watu kuanza kujitambua. Mungu azidi kukujalia afya njema.
"Niliwaambia ;wakati wao wako ndani ya land rover 109 kilomita arobaini nyuma yetu sisi tunaokimbizwa na kutuhumiwa kuhusu ugaidi na kupanga njama za kudhuru watu, wahusika halisi wa mambo hayo wako na Range Rover kilomita arobaini mbele yetu. Je,ni mwaka gani watawafikia na kuwaweka mbaroni hao jamaa?Hivi, kikosi cha IGP Mwema ambacho tumeelezwa ni maalum na kina makachero waliobobea kushindwa kurejesha mrejesho wa maana hadi sasa kwa angalau hata tukio moja, hivi watanzania hatushtuki tu? JK haushtuki ? Anyway,tuendelee kuwapa masurufu na kuwatengea mafungu tutaona! Sijui kama walinielewa au kumfikishia IGP Mwema huo ujumbe wangu"
 
Pole jembe, kamanda lwakatare yote yana mwisho ukomo wa magamba ndiyo unakaribia wanatumia mbinu cha kukidhoofisha chama chetu chadema. Tuko nyuma yako kamanda na tutapambana mpaka kieleweke. Aluta continua...
 
safi sana, makala nzuri mno.

kama ni kusafishwa basi Shekhe Ponda kwa mara ya kwanza leo amesafishwa vilivyo, nimeanza kurudisha imani kwa mbaali juu ya shekhe Ponda, bado natafakari.

Makala imejaa hekima nyingi na uhalisia wa asilimia kubwa i wish kila kiongozi, mwanachama, na mfuasi wa chadema angekuwa na maono kama haya na akayatekeleza bila unafiki basi wengi wangewaelewa chadema. Nakutakia maisha mema Lwakatale kwa maoni yako najua ni constructive kwa mustakabali wa taifa letu.
Ushauri: watu tusipende kuufukia ukweli japo unauma.

Pole sana,leo nimejua ni kwa nn CCM waliamua kukuchagua wewe kukuwekea kesi ya kutunga.Unaakili sana nimekumbuka hotuba yako bungeni wakati ukiwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni.Japo safari bado ngumu ila nina imani tutafika.

Hakika ujumbe huu umeniimarisha sana kuwa Chadema inatenda haki kwa nchi hii isipokuwa "Majini hayataki KUOKOKA, Sheikh Ponda alitoa jambo ambalo limebaki kichwani mwangu kama "ICON" kwamba huko "Uswahilini akina mama wa Kikristo na Kiislamu wanaachiana watoto wakienda sokoni mbona hakutokei vurugu hizi, nimebaki kutafakari kwamba wanasiasa wanahusika sana na vurugu za kidini hasa hawa wanaotuhumu chama fulani kuwa ni cha kidini wanatumia kulipua makanisa moto kuonyesha kwamba chama kimeleta mifarakano ya kidini kumbe ni wao wenyewe"
 
Hii makala Mwanakijiji hajaiona.Angeweza kutia neno hapo.Imesikitisha sana.Mungu atakusaidia
 
Pole sana kamanda Lwakatare,
Makala yako imekua shule tosha kwangu,nimejifunza mengi.
Kuna sehemu moja nimeshindwa kuelewa,swala la mtu kuwa na maadui na kutangaza hadharani bila kuwataja majina,sheria inasemaje hapo?Hilo sio tishio kwa kundi unalosema ni maadui zako?Hao wakipatwa na tatizo na tukisema unahusika wewe uliyesema una maadui utapona?Vipo wapi basi vyombo vya usalama?
Hilo ni fumbo na linahitaji utatuzi.Mbaya zaidi unatangaza hadharani kuwa una maadui,then jumapili unaenda kanisani kusali........UTUSAMEHE KAMA TUNAVYOWASAMEHE WALIOTUKOSEA........
Au maadui sio lazima wawe wamekukosea??????
 
Oh my Lord! I have spent more than 1 hour reading such sad and interesting story! But we still learn what was behind the scene !
 
Haya ni maneno mengi sana, na mengi ni ya kutafuta symphathy, au huruma, sisi wengine wetu itakuwa ni dhambi kubwa tukijaribu kumhukumu lwakatare wakati kesi yake ipo mahakamani.

Maandishi yote haya ni ya upotovu, na kujitetea kwa jamii, mimi kitu ambacho sitaweza kumsamehe au kukubali utetezi wowote wa lwakatare ni kwa hili jambo la kaa video, hali inajulika waziwazi kuwa ni cd ya ukweli na sio ya kuchakuchuliwa, alikuwa mzembe wa namna gani hata akareckodiwa, akiwa head of seurity, huyu bw hafai hata kidogo na yeye ndiye wakutueleza mambo yalivyi kuwa na atutoe hofu.

Hili lilomkuta ni lake yeye mwenyewe wala sio la chadema, kwenye chama kuna watu safi sana kama akina zitto nk.......
 
Lwakatare sikumfahamu vizuri kabla.Baada ya kusoma hii makala yake; nimegundua ni mtu mwenye Hekma,Mtafiti, Mtu anayejichanganya na jamii ya watu tofauti tofauti, mtu mvumilivu, mwenye busara za kadiri na mwenye vision.
 

Hakika ujumbe huu umeniimarisha sana kuwa Chadema inatenda haki kwa nchi hii isipokuwa "Majini hayataki KUOKOKA, Sheikh Ponda alitoa jambo ambalo limebaki kichwani mwangu kama "ICON" kwamba huko "Uswahilini akina mama wa Kikristo na Kiislamu wanaachiana watoto wakienda sokoni mbona hakutokei vurugu hizi, nimebaki kutafakari kwamba wanasiasa wanahusika sana na vurugu za kidini hasa hawa wanaotuhumu chama fulani kuwa ni cha kidini wanatumia kulipua makanisa moto kuonyesha kwamba chama kimeleta mifarakano ya kidini kumbe ni wao wenyewe"
cc: Mwigulu Nchemba
cc; Nape Nnauye jr
 
Last edited by a moderator:
MANENO MAKINI, KUTOKA KWA MTU MAKINI.!
pole sana lwaks..
nimedondosha machozi, seriously.!
kwakweli hatuna choise zaidi ya kuondoa mfumo na chama hiki dhalimu madarakani...
tusikubali kuona taifa letu lina megeka vipande vipande kutukana na udhaifu na tamaa ya watu wachache..
HAKUNA KULALA MPAKA KIELEWEKE.!!!!
siku zote uma ushinda dola dhalimu
 
Nimesoma post hii mstali kwa mstali. Mwisho, chozi limenitoka. Namafahamu huyo W.Lwakatare tangu tukiwa wadogo. Sikujua anaweza kuandika makala yenye funzo kubwa hivi. Pole sana kamanda. Mwenyezi Mungu akufariji wewe, mkeo na watoto wako. Vilevile, maandiko haya vyema wakayapata wanachama CHADEMA.

Sheik Ponda kumbe muungwana vile>>>>loh unaona sasa. At one time nilidhani ningeweza kukukimbia kama tungekutana nae uso kwa uso. Mungu ni wema.. katuonyesha ukweli

Kuhusu viongozi wa dini... ushuhuda na ushauri uliotolewa ni wa kweli. Achana kuwalamba miguu viongozi wa serikali weupe hao.

Pole sana W.L Kamanda
 
Mazungumzo kati ya Rwakatare na Shekhe Ponda pia ushirika wao kwa kipindi hicho cha siku zaidi ya 60 ukitafakazi kwa kina na kuchambua utajua kuwa jambo hilo linaeza kuleta mapinduzi makubwa sana katika siasa za Tanzania.
Chama cha Mapinduzi kimetumia sana udini katika kuikosanisha Chadema na waislamu. Lakini kulingana na maelezo ya Lwakatare kuwa Ponda ni mtu mwenye uelewa mkubwa tatizo hapewi nafasi ya kusikilizwa na dola,nahakika atakuwa amemsikiliza vema Rwakatare kama yeye alivyosikilizwa na baada ya hapo atapeleka ujumbe kwa wafuasi wake jinsi alivyo ielewa Chadema kupitia kwa LWakatare.
Ufahamu huo ukiingia mioyoni mwa waislamu juu ya Chadema ni wazi njama za CCM kwa kutumia udini hapo ndio mwisho na ni anguko kubwa sana kwao.
MIPANGO YA MUNGU HAITABIRIKI! ONA ALIVYOMKUTANISHA LWAKATARE NA PONDA GEREZANI KWA MAKUSUDIO MAALUM​.
 
Back
Top Bottom