Siasa si hisabati kwamba unapokokotoa formula vizuri unahakika na jibu, kuna ambao wamelaumu CDM kwa kutokuwa na wawakilishi lakini ukweli ni kwamba nchi inaongozwa na mfumo wa vyama vingi ambavyo vipo zaidi ya kumi na kila chama kinajitahidi kuangalia uwezekano wa kuchukua majimbo/kata na ndio maana unakuta kuna sehemu CUF amechukua na CDM haipo which means CUF wamecheza karata nzuri ya kukitambulisha chama chao.Pia lazima ujua kwamba vyama vinafanya kazi na wananchi ambao kila mmoja ana utashi wake hivyo tusiwalaumu CDM sana kama wadau wengine walivyochangia wakati
Ta Muganyizi amekuja na hoja ya kuwepo na way forward.
My take: Nadhani mkakati wa kwanza kwa CDM ni viongozi wa mkoa wa Kagera kwa ujumla bila support kutoka CDM taifa wafanye kampeni ya kuongeza idadi ya wanachama wapya katika wilaya husika maana kwa uzoefu wangu Bukoba kwa muda mrefu imekuwa ngome ya CUF kama chama cha upinzani maarufu hivyo imepelekea hata wilaya jirani ya Bukoba rural nayo kuwa ngome ya CUF. (Hapa Ta muganyizi atanirekebisha maana mie nilipita mitaa hiyo miaka ya 2000 - 2004 ambapo ukizungumzia upinzani unazungumzia CUF sijui siku hizi).
Mkakati wa pili ni CDM makao makuu kuangalia namna ya kusaidia viongozi wa CDM wa wilaya kifedha na kiufundi ili waweze kuwa na uwezo wa kuwafikia wananchi kwa kutumia raslimali chache zilizopo.
Mwisho, viongozi wa kitaifa kupita kama timu kupiga uhamasishaji wa nguvu na kuhubiri sera zao kwa uwazi ili waweze kufahamika kwanza kwa wananchi si unajua kama chama chenye nguvu ni CCM alafu kinachofuatia kwa umaarufu ni CUF hivyo ajenda hapa ni kupata mabalozi wazuri katika ngazi za vijiji na vitongojini (wanachama na wafuasi) ambao watasaidia kupeleka vuguvugu la siasa kwa wananchi kabla ya kuwaza ushindi katika ngazi ya kata.
Ukishakuwa na wachama na wafuasi wa kutosha inakuwa rahisi kwa chama kutambulisha vuguvugu la mabadiliko kwa wananchi kikubwa kwenye mikutano kusiwe na agenda ya siasa ya maji taka hasa kwa chama cha upinzani kilichopo eneo husika.