Wilaya nzima (Bukoba Vijijini) Hakuna CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wilaya nzima (Bukoba Vijijini) Hakuna CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ta Muganyizi, Oct 29, 2012.

 1. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #1
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Pamoja na maneno mazuri ya faraja kuwa Tanzania karibia inakombolewa...bado napata mashaka na mbinu za Ukombozi tulizonazo. Huwezi Kuamini kinachoendelea katika baadhi ya Wilaya nchini.....ambapo yaani hata harufu ya CDM kuisikia ni kwa machale.

  Nilibahatika kuingia katika kikao cha Madiwani Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba (Rural) yenye kata 29 nilisikitika kuona kuwa kati ya hizo kata 29, kata 28 zinaongozwa na CCM na kata moja tu ya Katoro inaongozwa na CUF. Yaani hapa upinzani umeoneshwa na CUF pekee japokuwa bado na yenyewe haitoshi.

  Wakati kikao kianendelea Viongozi wa Vyama vya upinzani walikuwa wanakribishwa kuhudhuria kikao hicho. Waliokaribishwa ni Viongozi wa CCM na CUF kwa siku ya kwanza. Siku ya Pili alihudhuria wa CCM na NCCR Mageuzi na CUF. Ikabidi niulize; imekuwaje NCCR Mageuzi wamefika hapa wakati hawana hata Kata moja? Jibu nililopewa ni kuwa "angalau NCCR wanaonekana as chama cha Upinzani, hata kama hawana kata hata moja wao ni "ACTIVE" maeneo haya. Baada ya hapo nikajiuliza inakuwa je Chama kinachopigiwa chapuo kuchukua nchi hakina jitihada yoyote ili kijihakikishie ushindi?

  Nimewahi kusema hapa kuwa CDM hapa Bukoba mjini haionekani.......hatuoni initiative zozote za kukipromote chama. Viongozi wa Mkoa wako wapi? Niliwahi kusema Chama kama chama kiitishe mkutano wa wanachama wake kioneshe mpango kazi wake kama tatizo ni la ki budget wanachama wenyewe tujipange na kukiwezesha kuwafikia wananchi lakini wapi. Ofisi au Makao makuu naambiwa ni Ijuganyondo.....pembeni mwa mji. Hata kutoonekana kwa ofisi mjini ni udhaifu........

  Tatizo nini? Inawezekana kuna wilaya Nyingine CDM haina hata kata moja!! Naomba tena Uongozi wa CDM ueleze kinaga ubaga nini mpango wake wa Kukiimarisha chama Mkoani Kagera .,....Hususan Wilaya Hii ya Bukoba? Siwezi kuwasemea wengine hapa nchini. Naomba anayeona kulegalega kwa CDM mahali pake aombe ufafanuzi kwa viongozi ili watoe majibu ya pamoja. Nisipojibiwa kwa hili siongei tena.

  Nasuburi maelezo hapa........tumejiuliza wengi ...tunasubiri majibu na makakati.
   
 2. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #2
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kama CDM ni active na haikukaribishwa.....basi watuoneshe ua ctive wake uko wapi. Yaani inasikitisha. Mpango na mkakati bado ni dhaifu
   
 3. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Kama Wliya nzima hakuna hata CDM mmoja hivi Wlifred Rwakatare anatokea wilaya gani naomba kukumbushwa.

  Hivi ulitegemea CCM wawaalike CDM kweli Ta Muganyizi hivi ni nshomile kweli huwezi kuona huo ukweli dhahiri.

  CUF imefunga ndoa na CCM huko ZNZ. JK Rais wa JMT amemteua Mbatia mwenyekiti wa NCCR kuwa mbunge wa kuteuliwa.

  Kwa CCM vyama vya Upinzani ACTIVE vinavyonekana ni CUF, NCCR, UDP etc. CDM kwa CCM ni chama cha msimu kisichokuwa na nguvu. Tia akili kichwani nshomile.
   
 4. bhikola

  bhikola JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 457
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  huko si anakotoka lwakatare yule mwanasiasa, sijui jina la kwanza nani alikuwaga mbunge wa cuf au, si nilimuona juzi nyololo akiwa kwenye movement for chura?
  mwambieni charity beggins at home
   
 5. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #5
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Usichanganye mambo. Mie naongelea Bukoba Rural as District. Wengi wenu huwa mnachanganya Bukoba kama Mkoa Mkoa ni Kagera.....na Kuna Wilaya Nane ikiwemo Bukoba Municipa na Bukoba(Rura) District.

  Ki mamntiki ni kuwa kwenye vikao vya madiwani kama walau Chama kina kata moja basi Kiongozi wa Chama husika hualikwa.........wewe tulia tujenge chama chetu. Mbona kwenye vikao vya Manispaa CDM hualikwa. Toa mchango wako tufanyeje walau tupate kata moja.

  RWAKATARE ni wa pale Kibeta Bukoba Municipal. Nikukumbushe tena nimesema Bukoba Rural
   
 6. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #6
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Hiyo Movement for Chura siijui. Kuhusu Charity to begin at home ni sawa lakini awashirikishe viongozi wa Kitaifa alionao aje na mpango kamili.
   
 7. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #7
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tuache kulalamika, tuchukue hatua, kama wewe ni bukoba vijiji chukua jukumu la kujenga chama kwenye wilaya yako! Usisubiri watu wengine hata kama wapo! Utajicheleweshea mabadiliko!
   
 8. T

  Thesi JF-Expert Member

  #8
  Oct 29, 2012
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Unachokisema kina mashiko na changamoto kwa wanachama wa CDM. Lazima chama kibuni mikakati ya kuingia nchi nzima. Wanachama tuissupport.
   
 9. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #9
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Ndio ujiulize kura zipi za urais zilizochakachuliwa 2010 ikiwa baadhi ya maeneo hawana uwakilishi au wingi wa wanachama? tatizo CDM wanajidanganya na kelele za mashabiki majukwaani .
   
 10. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #10
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Ta Muganyizi, tatizo la aina hiyo haliko Bukoba Vijijini tu hata Muleba Kaskazini ni hivyo hivyo. Mimi natokea Kamachumu.Kule tangu Mzee Christopher Ngaiza afariki, pamekosekana kiongozi dhabiti wa CDM. No meetings held at all at least to addess the pressing issues of the day and get the wananchi there usher their opinions as how to resolve them. Haonekani mtu kule anaweza kuongea lugha ya wananchi na kuwapatia ufumbuzi. Kuna tatizo la over satisfaction ambalo Jenerali Ulimwengu aliwahi kulielezea kuwa Waafrika moja ya sifa tulokuwa nayo ni kulidhika kuliko pitiliza tena kwa mafanikio ya siku moja. Nina wasiwasi CDM wengi wasije wakalewa sifa za jumla za mikutanoni na kwenye maandamano na labda pengine wakafikiri kuwa kwa kuwa Dr.Slaa anafanya kazi mchana na usiku kukieneza chama basi nao watatbebwa na sifa hizo. Si hivyo, wale ambao are aspiring for leadership come 2015 wanatakiwa kufanya penetration to the masses. Walipo viongozi wa CDM amabao watapata kuona uzi huu kule Muleba Kaskazini tunaomba mbadala wa Balozi Ngaiza who did an excellent job worthy emulation. Mbali na kukijenga chama bali alenda mbali kwa kuetengeza ajira nyingi kupitia hotel-Kamachumu Inn, Kiwanda cha kutengeneza maji ya kunywa na bakery facility. Watu wengi waewekeza nje ya Kagera lakini aliona charity ianzie nyumbani. Namna ya kumwenzi ni kutupatia mtu mbadala
   
 11. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #11
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Mke wa fake president Josephine Mushumbuzi akaweke kambi Bukoba kunusuru aibu.
   
 12. Mingoi

  Mingoi JF-Expert Member

  #12
  Oct 29, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 10,636
  Likes Received: 2,344
  Trophy Points: 280
  Siku mambo yakibadilika Moshi na Arusha ndio watajua taifa la Tanzania linaundwa na vijiji,kata,tarafa,wilaya na mikoa yote.
   
 13. B

  Bigaraone JF-Expert Member

  #13
  Oct 29, 2012
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 722
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35


  Ta Muganyizi hajalalamika lakini amesema kitu bila kumungunya maneno. Huwezi ukakuruka from nowhere ukaitisha mkutano na ukasema unajenga chama. There must be pedestral from which you can air your views and support the party. Hiki ndicho anachokililia Ta Muganyizi. Something must be put in place from which wanachama will convey the message.Short of that, there will be chaos and do not rule out human nature as there can happen people who aspiring for leadership in the near and distant future wanweza wakasema umeingilia ngome zao. Lakini kikienda kama chama hayo mambo hayatakuwepo na anayejitolea anakuwa na party strategies at heart and will implement them depending on the environment
   
 14. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #14
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Kwa mamlaka yapi wewe. Nchi hii kwa sasa ina utawala. Nataka tuliowapa dhamana walitekeleze hili. Ndo maana nikashauri kama tatizo ni budget tushirikishane.
   
 15. d

  dotto JF-Expert Member

  #15
  Oct 29, 2012
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Changamoto ziko nyingi pamoja na huyo sjui Mingoi kushambulia watu binafsi na maisha yao but: ebu fikiria mbinu ovu zinazotumiwa na CCM kuizima Chadema popote pale inapotia mguu. Mfano. ni Morogoro na Iringa. Mungu yuko na anajua mahala CCM itakapofia na iko siku yaja maana nchi hii sio mali ya CCM ni mali ya Mungu mwenyewe.
   
 16. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #16
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Bora umelielewa hili mkuu.......cha kushangaza hapa anaweza asitokee kiongozi hata mmoja akalisemea hili. Wasipokuwa serious itabidi tuwaache wajifunze kwa vitendo japokuwa mabadiliko yatachelewa.
   
 17. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #17
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  [h=5]Nzi na nyuki hufa kwa kulazimisha kupenya kwenye kioo , ndivyo watakavyoangamia wasomi, wafanyakazi na wakulima wanaolazimisha kutimiza ndoto zao kupitia CCM, sasa tuko kwenye kampeni maalum dhidi ya ccm 2015, waliingia kwa mbinu watatoka kwa mbinu watenda hutendwa, tuisaport CHADEMA, Tanzania bila ccm Inawezekana! Tuma ujumbe huu kwa waliochoshwa na ccm hasa wakulima, walimu, NMB,TRL, Wazee Wa EAC na Wanafunzi Vyuoni.MUNGU ibariki CHADEMA DAIMA_xx2[/h]
   
 18. Ta Muganyizi

  Ta Muganyizi JF Gold Member

  #18
  Oct 29, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 5,134
  Likes Received: 413
  Trophy Points: 180
  Niambie vilevile la kumueleza Mke wa Orijino president Salma la kumueleza mmewe walau kila mtoto wa primary nchini akalie dawati.......ili kunusuru aibu ya nchi yenye raslimali zote hizi ikiwa na misitu minene wanafunzi kukaa chini wakiwemo wa Chalinze na Pwani ndani ndani
   
 19. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #19
  Oct 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 4,971
  Likes Received: 666
  Trophy Points: 280
  Mkuu umewashtua lazima wata take action isije ikawa ukombozi tunauzungumzia mijini mwaka 2015 tukachota aibu tele. Tusiridhike CDM tukaze buti licha ya kwamba serikali inapambana nanyi utafikiri wanapambana na alqaida. Nataka niamini kuwa serikali imekidhoofisha sana CDM hasa kuanzia matukio ya morogoro na iringa. Spidi imepungua sana na kwa hili wamefanikiwa. Ushindani unaokuja wa kugombea urais 2015 ni wa kudhoofisha mikutano ya CDM huko mabogas wa CCM wakiachwa kupeta kuhutubia bila kubughudhiwa. Hi ni sawa na vita ya kushindanisha timu mbili moja na washabiki ikiwa nuruni na nyingine isiyo na washabiki kuwa gizani. Then unawaambia washabiki waamue mshindi ni nani? Its crazy politics
   
 20. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #20
  Oct 29, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,700
  Trophy Points: 280
  Mkuu pale Bukoba siasa zimechanganyika na UDINI, nilifika pale nikaingia kwenye ofisi moja ya CUF iko opposite na Manyema Hotel, mtaa wa pili opposite na zilipo office za TRA na TTCL kwa bahati nzuri nilikuwa nimevaa kanzu ya kiislam, nikaingia ofisini kujuliana na "jamaa zangu katika imani" waliokuwa wamefurika pale ofisini. Stori zao ni kuisema Chadema tu na sio CCM, lakini pia walikuwa wakiisema Chadema katika namna ambayo si ya ubaya bali walichokuwa wakikitaka ni kuwa Chadema igeuke na kuwa chama cha kutetea madai yao. Hata wao walionyesha kuvunjika moyo na progress hafifu za CUF.

  Nilifika mitaa ya Kahawa guest na Gerida Guest, kwa mbele kuna hotel na bar inaitwa Lily kama sikosei, vijana wanajadili udini tu na wakijadili siasa wanajadili katika Muktadha wa kidini tu. Angalau kidogo kama unaenda mitaa ya Rwamishenye ukipita Hamugembe unaweza kuona mchanganyiko wa watu na mitazamo tofauti.

  Kwaiyo TaMuganyizi utakubali kuwa pale bukoba mjini kuna idadi kubwa sana ya waislam type ya wale wa Buguruni, ambao wakielezwa jambo na kiongozi wao yeyote wa dini bila hata kulichuja wao wanaamini na kufuata Mkumbo. Siasa za Bukoba mjini zimeshaathiriwa na Udini
   
Loading...