Wilaya na Shule zakabidhiwa bendera nyeusi

Wilaya na Shule zakabidhiwa bendera nyeusi

Mzalendo_Mkweli

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2012
Posts
2,068
Reaction score
1,332
Katika gazeti la Mwananchi la 22/02/2018 nilisoma makala inayohusu mkuu wa mkoa wa Dodoma kukabidhi bendera nyeusi kwa wilaya pamoja na shule ambazo zimefanya vibaya katika mitihani ya Sekondari na Primary. Baada ya kusoma hiyo makala na kufanya tafakuri kwa muda nimeona niwaulize ninyi wadau juu ya mtizamo wenu juu ya aina hii ya adhabu/rewards ambayo mkuu wa mkoa wa Dodoma ameibua. Je aina hii ya utoaji wa zawadi/adhabu inaweza kuwa na tija kama itaigwa na wakuu wengine wa mikoa?

Nawakilisha
 
Mkuu hauoni kama hii ni njia ya kiustarabu ya kuwahimiza wakuu wa wilaya na shule husika waongeze bidii?

Ahsante

Bendera nyeusi maana Yake ni kuuzika huo mkoa.

Nilijua watapewa vifaa vya kufundishia na kuongezewa waalimu(kama kuna uhaba)
 
Ukiona elimu inasuasua ujue kuna mengi yalisuasua hence yakadhoofisha elimu! Bendera nyeusi haiondoi ukweli kuwa waalimu wana changamoto nyingi,haiondoi ukweli kuwa elimu bure ni elimu inayolazimisha watu Waende shule bila kujali wanachoenda kukipata huko!

If so basi hiyo bendera isiishie huko tu,bali iende hadi kwenye huduma ghali na mbovu za afya,iende kwenye demokrasia mbovu,iende kwenye uchumi usiomsaidia mwananchi! Mwisho wa siku hiyo bendera nyeusi itakuwa bendera ya taifa!! Maana ina fit kila kona ya nchi hii!! Shughulikieni changamoto za elimu na si kuzifunika kwa bendera nyeusi, ikulu yetu basi ipewe bendera nyeusi na nyekundu!!
 
Watatue changamoto mashuleni, walimu wana shida nyingi sasa mabendera ndo yafanye nini
 
Tuna safari ndefu kufikia ndoto tuitakayo kama kiongozi anashindwa kujua kiini cha tatizo na kukimbilia cheap publicity.

Ningemuona ana akili/busara kama angefanya initiatives na wadau wa elimu kuona namna wanatatua changamoto za elimu, as long as mtoto hayuko mbali na baba yupo sahihi kwa wakati wake.
 
Kama bendera nyeusi inafaa kupelekwa walikofanya vibaya, basi, nashauri hili jambo lisiishie ktk mikoa au wilaya, liwe la kimataifa, ili hata nchi zinazofanya vibaya zipewe hiyo!
Hata "matawini" ipepee hiyo
 
Katika gazeti la Mwananchi la 22/02/2018 nilisoma makala inayohusu mkuu wa mkoa wa Dodoma kukabidhi bendera nyeusi kwa wilaya pamoja na shule ambazo zimefanya vibaya katika mitihani ya Sekondari na Primary. Baada ya kusoma hiyo makala na kufanya tafakuri kwa muda nimeona niwaulize ninyi wadau juu ya mtizamo wenu juu ya aina hii ya adhabu/rewards ambayo mkuu wa mkoa wa Dodoma ameibua. Je aina hii ya utoaji wa zawadi/adhabu inaweza kuwa na tija kama itaigwa na wakuu wengine wa mikoa?

Nawakilisha
Lakini nilisahau kuuliza, Ana vyeti?
 
Akili za mkuu wa mkoa nadhani uwezo wake ume -xpire badala ya kuongeza walimu na vifaa katika mashule yeye anabuni bendera nyeusi,kweli hii ndo Tanzania ya viwanda
 
Back
Top Bottom