Abunwasi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 5,486
- 3,470
Mimi nimeisoma vizuri ripoti ya richmond na ukweli ni kwamba hakukuwa na kamati ya tanesco bali kulikuwa na kamati kuu ambayo mlikuwa na wajumbe toka tanesco, wizara ya nishati, mwanasheria mkuu, wataalam wa uchumi na pia kulikuwa na kamati ndogo ndogo ambazo zilikuwa ni za ufundi, sheria nk. kamati kuu ambayo ilikuwa chini ya waziri mkuu ndiyo iliyotoa mapendekezo ya majumuisho ambayo waziri mkuu ndiyo aliyoyawasilisha kwenye baraza la mawaziri. Hata baada ya serikali kuridhia hilo [baraza la mawaziri] wakati wa utekelezaji wa mradi huo kuna mapungufu yaliibuka ambayo yalimshtua WM na alimuarifu mkuu wa kambi juu ya anavyoona na hatua ambazo alitaka kuchukua dhidi ya mapungufu hayo. Kwa vile mkuu wa kambi alikuwa nje ya nchi, WM aliombwa avute subira hadi atakaporejea ili suala hili lijadiliwe kwenye baraza na ndipo hapo mandumila kuwili walipo leak mambo hayo na kufanywa kama kashfa inayomhusu WM.