Maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama kitaifa yanaanza leo huko mkoani mbeya.
Dar es salaam tumeianza wiki hiyo kwa foleni ndefu sana bararani, hasa sisi watumiaji wa njia ya ali hassan mwinyi.
Kwa mtizamo wangu nlidhani kuwa wiki hii ndio ingekuwa haina foleni kwani ndio ingekuwa wiki muafaka kwa askari wa usalama barabarani kuonyesha mbinu ambazo wamekuwa wakizitafiti ili kupunguza kero ya msongamano dar es salaam (nsiongee sana, huenda hawana hata mpango wa kutafiti namhna ya kuzipunguza hiziz foleni)
Poleni jamani!kwa foleni natumai wazee wa feva watajitahidi kuwa imara katika kusimamia foleni japo iende fasta fasta. Nipo morogoro hapa shamrashamra za wiki ya nenda kwa usalama hapa sio kubwa sana japo hawa wazee wa feva wamejitahidi kutanda barabara zile muhimu muhimu na pia ukaguza mdogomdogo! sasa siju kama ndo watafuata maadili au itakuwa kama kawaida.
Hawajui kuwa wakikamata madereva waovu yaani wanaotanua, waliolewa, wasio na leseni, daladala zinazosimama pasipo vituo polisi ingetengeneza pesa kibao za faini za papo kwa papo.........na amani barabarani ingekuwepo
wiki yaENDA kwa usalama ndizo ripoti zitakavyoandika.
Ila amin amin nakuambieni kwamba bila teknolojia na kuboresha barabara zetu hakuna jipya ktk kupunguza msongamano wa magari ktk jiji.
Kingine mkitaka kuona msongamano unapungua ni kuwashinikiza wateule wetu wahamie dodoma kwani wanatuwekea kiwingu hapa mjini tushawachoka na tambo zao na foleni ndefu za kumsubiri mtu mmoja apite na vimwelumwelu huku tunaomlipia kodi tunateseka