Wiki ya kusulubiana Dodoma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wiki ya kusulubiana Dodoma

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Makaayamawe, Nov 2, 2009.

 1. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #1
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Wiki ya kusulubiana Dodoma

  Na Mashaka Mgeta
  2nd November 2009

  [​IMG] Joto la Richmond lapanda hadi asilimia mia
  [​IMG] Kamati ya Mzee Mwinyi ana kwa ana na wabunge
  [​IMG] Takukuru waendelea kuwawinda wabunge


  [​IMG]
  Bungeni.

  Wakati mkutano wa 17 wa Bunge ukiingia wiki ya pili leo, wiki hii inatarajiwa kutawaliwa na mikiki mikiki mingi kutokana ajenda kuu nzito kutarajiwa kujadiliwa.

  Mambo ambayo yatautikisa mkutano huo ulioanza Oktoba 27, ni pamoja wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kukutana na Kamati iliyoundwa na Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kumaliza uhasama baina yao na dhidi ya serikali.

  NEC ya CCM iliunda kamati hiyo Agosti mwaka huu kwa ajili ya kuchunguza malumbano yanayotokea katika Bunge na katika Baraza la Wawakilishi, leo inatarajia kukutana na wabunge mjini Dodoma.

  Kamati hiyo iliundwa kutafuta chanzo cha uhasama wa wabunge miongoni mwao na dhidi ya serikali na ule wa Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi dhidi ya serikali ya Muungano, inaongozwa na Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, ikiwa na wajumbe, Pius Msekwa (Makamu Mwenyekiti wa CCM –Bara) na Spika wa zamani wa Bunge la Afrika Mashariki, Abdulrahaman Kinana.

  Katika Mkutano uliopita wa16 wa Bunge na wa Baraza la Wawakilishi, Wabunge waliwashambulia mawaziri wengi wakati wa kujadili bajeti ya mwaka huu wa fedha 2009/10.

  Pia Wajumbe kadhaa wa Baraza la Wawakilishi walielekeza mashambulizi yao kwa baadhi ya mawaziri wa serikali ya Jamhuri ya Muungano, akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kiasi cha wengine kutaka akapimwe akili.

  Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi walizungumza kwa jazba wakati wa kujadili masuala ya umiliki wa mafuta na gesi asilia pamoja na kauli kadhaa ambazo zimekuwa zikitolewa na Waziri Mkuu kuhusu hadhi ya Zanzibar kama ni nchi au la. Kamati hiyo imeshakutana na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika kikao kinachoendelea mjini Zanzibar.

  Kamati hiyo jana ilikutana na Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM mjini Dodoma katika kikao kilichoanza asubuhi na kuendelea baadaye mchana.

  Hakuna taarifa rasmi zilizopatikana juu ya kilichojadiliwa. Hata hivyo, habari zinaeleza kuwa Mwinyi na kamati yake walijitambulisha kwa kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM na mambo watakayojadiliana na wabunge wote wa chama tawala leo.

  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa NEC, Kapteni John Zephania Chiligati, alithibitisha kufanyika kwa kikao cha jana kati ya Kamati ya Mwinyi na Kamati ya Uongozi ya Wabunge wa CCM.

  Hata hivyo, Kapteni Chiligati alikataa kueleza kilichozungumzwa katika kikao hicho.

  Kikao cha leo kinatarajiwa kufanyika jioni baada ya mkutano wa Bunge kuahirishwa.

  Hata hivyo, habari ambazo Nipashe ilizopata kutoka Dodoma jana jioni zinasema kwamba, Kamati ya Mzee Mwinyi ilikutana na wenyeviti wa kamati za Bunge wanaotoka CCM ili kuwaeleza madhumuni ya ziara yao.

  Mtoa habari wetu alisema kwamba wenyeviti hao walielezwa ili nao wawaeleze wajumbe wa kamati zao, ili kupunguza joto la malumbano leo wakati wa kukutana.

  Wakati kamati ya Mwinyi inakutana na wabunge kwa lengo la kurejesha nidhamu ndani ya CCM kama ilivyoagiza NEC, mwisho wa wiki hii hoja zinazohusu mkataba tata kati ya kampuni ya Richmond Development (LLC) na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) na kuadabishwa kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), zitatikisa Bunge.

  Hatua hiyo inatokana na hoja hizo kutakiwa kuwemo katika taarifa ya serikali kuhusu utekelezaji wa maazimio 23 yaliyopitishwa na Bunge mwaka jana, ikiwemo kuwachukulia hatua wahusika katika kashfa hiyo.

  Wahusika waliotajwa ni pamoja Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk. Edward Hoseah, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na Katibu Mkuu mstaafu wa Wizara ya Nishati na Madini, Arthur Mwakapugi.

  Mwanyika na Mwakapugi wamekwisha kustaafu na nafasi zao zimekwisha kujazawa.

  Kustaafu kwao ingawa ni kwa mujibu wa sheria, kumewafanya baadhi ya wabunge wahoji kasi ya serikali katika kutekeleza maazimo yake huku watuhumiwa wakimaliza utumishi wao bila kuchukuliwa hatua zozote.

  Wakati wa Mkutano wa 16 wa Bunge, ripoti ya serikali ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu Richmond ilikataliwa na kutakiwa kuwasilisha nyingine wakati wa mkutano huu.

  Kuna uvumi kwamba Bunge linalitarajia kumaliza mkutano wake wiki hii, litaongezewa siku hadi mapema wiki ijayo ili kutoa fursa kwa mambo nyeti kujadiliwa kwa kina.

  Ingawa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, ameshasema kuwa, taarifa ya serikali kuhusu Richmond itawasilishwa na kujadiliwa keshokutwa, baada ya kuwasilishwa kwa miswada iliyopangwa kwa mkutano wa 17 wa Bunge unaoendelea, lakini kuna taarifa kuwa mkutano huo huenda ukaongezewa muda wa siku mbili zaidi.

  Wakati mjadala kuhusu Richmond ukisubiriwa, taarifa zinadai kuwa wabunge wamejiandaa kuhoji sababu za kutochukuliwa hatua kwa Dk. Hoseah ambaye taasisi yake inaendesha zoezi la kuwahoji wabunge kuhusu kupokea posho zaidi ya mara moja.

  Wabunge kadhaa wameshaonyesha kutoridhishwa na kitendo cha kuhojiwa na Takukuru wakati ambapo Bunge linasubiri utekelezwaji wa maazimio yake, ikiwemo Dk. Hoseah kuchukuliwa hatua. Dk. Hosea anahusishwa na utoaji wa taarifa potofu kwamba hapakuwa na vitendo vya rushwa katika mchakato wa kuipa Richmond ushindi wa zabuni ya kufua umeme wa dharura wa megawati 100 mwaka 2006 wakati nchi ilipokumbwa na ukame na kusababisha kukauka kwa maji katika mabwawa ya kuzalisha umeme.

  Hatua hiyo ilikuwa tofauti na kilichobainishwa na Kamati Teule ya Bunge iliyofanya uchunguzi nje na ndani ya nchi kuhusu kampuni ya Richmond.

  Mbunge wa Kyela, ambaye pia alikuwa Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dk. Harrison Mwakyembe, alilithibitishia Bunge kuhusu viashiria vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kutawala mchakato wa kutoa zabuni kwa Richmond.

  Kashfa ya Richmond ilisababisha aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na waliokuwa mawaziri wa Nishati na Madini kwa vipindi tofauti, Dk. Ibrahim Msabaha na Nazir Karamagi kujiuzulu Februari mwaka jana kutokana na kashfa hiyo.

  Hayo yakiendelea, Takukuru nao wanadaiwa kujipanga kuwahoji baadhi ya wabunge wanaodaiwa kuchukua posho mara mbili kwa kazi moja.

  Jana gazeti dada la The Guardian On Sunday lilimkariri Dk. Hosea akisema wataendelea na kazi ya kuwahoji wabunge na kazi hiyo haijasitishwa.

  Msimamo wa Takukuru unaelekea kuzidisha msigano na wabunge, baadhi wakiwa wamesema wazi hawatakubali kuhojiwa, hoja inayoungwa mkono na Spika wa Bunge, Samuel Sitta.


  CHANZO: NIPASHE
   
 2. Kaitaba

  Kaitaba JF-Expert Member

  #2
  Nov 2, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 928
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Watanzania sijui tukoje!!!, we hauoni kuwa hakuna chochote kinachoendelea zaidi ya kujadili posho mbili za wabunge???!!!

  au na wewe ni miongoni mwa wanaotuzuga tujue kuwa dom kuna chochote. KALAGABAO
   
 3. Makaayamawe

  Makaayamawe JF-Expert Member

  #3
  Nov 2, 2009
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 341
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaitaba,
  Nakubaliana na wewe kabisaaa. Hii inaweza ikawa ni kalagabao. Wabunge wakifanya kazi yao (kuihoji serikali) kama inavyowajiri wanaambiwa kuwa ni utovu wa nidhamu. Kwa hiyo sio ajabu wakajadili posho badala ya Richmonduli. Tutafika kweli?
   
Loading...