Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 578
- 2,613
Wiki ya Chanjo Duniani (World Immunization Week) huadhimishwa kila mwaka kwenye wiki ya mwisho ya mwezi Aprili ili kuongeza Ufahamu wa Umuhimu wa Matumizi ya Chanjo katika kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali.
Chanjo hutengenezwa kwa kutumia Vimelea viliyo dhoofishwa ambavyo baada ya kuingizwa Mwilini, huamsha Kinga na kuufundisha Mwili namna Sahihi ya kupambana dhidi ya Maambukizi ya Ugonjwa husika.
Baadhi ya Chanjo hutolewa kwa dozi 1 huku zingine zikihitaji dozi nyingi kutengeneza Kinga Kamili.
Kupitia njia hii, Mwili hutunza Kumbukumbu za namna Bora ya kujilinda pindi utakapo Shambuliwa na Vimelea hivyo siku za Usoni.
Hadi sasa, Chanjo huzuia zaidi ya magonjwa hatari 20 pamoja na kuzuia vifo vya takriban watu milioni 5 duniani kila mwaka.
Tangu kugunduliwa kwa chanjo ya Kwanza yenye mafanikio mwaka 1796, Chanjo zimetoa mchango mkubwa katika kupambana na majanga ya kidunia yaliyotokea kwa nyakati mbalimbali.
Baadhi ya Magonjwa yanayoweza kuzuiliwa kwa chanjo ni Kifua Kikuu, Polio, Pepopunda, Kifaduro, Dondakoo, Homa ya Ini, Magonjwa ya Uti wa Magongo na Kichomi yanayosababishwa na Haemophilus Influenza, Surua, Nimonia, Homa ya Uti wa Mgongo, Magonjwa ya Kuharisha pamoja na Saratani ya Mlango wa Kizazi.
Chanzo: WHO