Wigo wa kodi uendane na majibu ya kitafiti

mbenge

JF-Expert Member
May 15, 2019
4,573
9,809
Leo nikiwa maktaba, nimebahatika kupitia "Organisation Chart" ya TRA. Pamoja na mambo mengine nilivutiwa na muundo wake katika sehemu ya "Department of Research & Policy". Niliweza kujifunza ya kwamba, Tafiti na Sera ni idara yenye kuwajibika zaidi katika uongozi wa juu na kujikita zaidi katika kumsaidia CG katika masuala yenye kuhusu "fiscal policy" (ninaweza kusahihishwa hapa).

Lakini jambo moja ambalo nimeliona hapo, ikiwa kama "knowledge gap" ni kuhusisha tafiti katika mambo ya sera tu. Nafikiri, katika muundo wake, TRA ingalipaswa kuwa "Department of Research & Development" na ndani yake ingegawanyika ktk "subdivisions" za "Policy, Taxpayer Education, Institute of Tax Administration and the likes".

Nafikiri hivyo kwa kuwa, ili tupate kuwa na effective tax base, ni lazima tupate majibu ya kitafiti kuhusu urafiki wa viwango vya kodi zilizopo kwa wadau, mazingira rafiki ya ukusanyaji wa kodi husika na pia kufanyia kazi malalamiko yaendanayo na kodi. Na jambo hilo linaweza kufanikiwa endapo Idara hii itashuka zaidi katika ofisi za kikodi za wilaya.

Idara hii ya R&D, ingaliweza kuwa ndiyo mratibuji, mtafutaji na mtambuaji wa kodi zote ambazo zimejificha kupita uwezo wa wigo wa kodi uliopo, hasa katika biashara nyingi ambazo zipo katika sekta isiyo rasmi.

Ni kweli wigo wa sasa huzikaba koo barabara biashara zilizopo katika sekta iliyokuwa rasmi, huku ukiziiacha zile zizizo rasmi zikitanua katika "extra legal environment". Sehemu kubwa ya biashara zilizo rasmi hufanya kazi sambamba na masaa ya kawaida ya muda kazi wa idara nyingi za TRA. Hufunguliwa asubuhi na kufungwa jioni, na nyingi zipo ktk maeneo ambayo Maafisa wa TRA huyatambua na kuweza kuyafikia.

Endapo, Idara ya R&D ingejitanua na kushuka chini hadi ofisi za Kodi za kiwilaya, wangaliweza kufanya tafiti na "mobile offices" tena kwa masaa 24, na kuja na majibu yenye kuonyesha kodi zinazopaswa kukusanywa, pasipo vizingiti vya muda wa kazi, usiku ama mchana, urasmi ama kutokuwa rasmi kwa biashara husika, makadirio sahihi kuendana na vipato sahihi vya wenye kuendesha biashara hizo.

HITIMISHO:
Mimi siyo mbobezi katika masuala ya kodi, hivyo nimeileta mada ili niweze kuchokoza wataalamu na magwiiji wa mambo hayo waweze kuyanyambua kwa weledi zaidi kupitia jukwaa hili. Nimefanya hivyo kwa kuwa naamini R&D inajikitika chini zaidi kwenye "technical level" zaidi ya ilivyokuwa sasa ambapo ipo zaidi kwenye "abstract level".
 
Mkuu nadhani haya yanawezekana dunia ya kwanza
Mkuu, katika maeneo nyeti ambayo nikiwa likizo siachi hata mara moja kuyafanyia kaz,i mojawapo ni hili lenye kuhusiana na kodi. Kila kitu kinawezekana, wala si suala la waliiopo katika dunia ya kwanza. Ni suala la uamuzi tu na kutoa " priority" ambayo nayo pia ni "research based" Si suala la kukimbizana na kujibishana na watu mliopo katika kambi tofauti za kiitikadi na kisiasa.
 
Back
Top Bottom