Wifi yangu amezidi

wanasema tenda wema nenda zako usingoje shukrani

undugu kazi sana...........mimi binafsi nilisadia ndugu wengi sana na leo wana nafasi zao....sasa hivi wakija dar wanafikia hotelini kwangu hawafiki utasikia tu fulani alikuja dar, hakufika kwako?....mimi huwa sijali na nilipokuwa nawasaidia sikutegemea malio yoyote......mke wangu alikuwa na moyo kama wa huyu mleta mada hapa alikuwa anaumia kweli kuona jamaa hawafiki nyumbani...nikamwambia waache tu maana geti liko wazi wanakaribishwa ila kwa kweli inaudhi kiasi flani......

huyu wifi yako katika maisha yake hakutegema kupata kazi kama hiyo...kwa kifupi hana tabia nzuri hasa hiyo ya kukutupia bia moja moja.....we endelea na kazi zako dada yangu achana nae......
 
Jamani mwenzenu na wifi yangu mke wa kaka angu baada ya kuukwaa Ukurugenzi huko Dodoma ameanza nyodo zilizo pitiliza wakati nilimpokea mwenyewe mjini kaja kujiendeleza kimasomo Chuo kikuu na tulikuwa tunakula dagaa leo hii amepata ukurugenzi anasema hawezi kabisa kufika kwangu anataka alale guest nilipo muuliza mbona pakulala nimekuandalia akasema hadhi yake hawezi kabisa kulala kwangu mitaani pale guest bei gani chumba nikamwambia zipo za Tsh.10000-30000/= akasema hakuna guest yenye hadhi ya kulala yeye akaniambia anaenda Sinza kulala kwenye guest za hadhi yake kwakweli ubinadamu kazi jamani.


Wote wawili muna matatizo yanayofanana..

Wewe ulitegemea kuheshimiwa sana kwakuwa uliwahi kumsaidia pengine ulikuwa na maneno maneno wakati huo..

Yeye ni limbukeni asiye weza ku control success??

Hapo ulipo unasubiri afeli ufurahi ili muwe pamoja (uchawi)...

wote nyie mna matatizo jitazameni
 
Julieth, mengi yameshasemwa hapa na wanaJF. Kilichobaki usijali, piga moyo konde usonge mbele na maisha yako. kama kakataa kuja kulala kwako ni vema pia maana kakupunguzia tabu za kumfikiria umpikie nini mgeni kwa siku atakazokaa hapo kwako. Usitegemee shukrani kutoka kwa binadamu mwenzio hata kama ni ndugu yako maana ndugu saa zingine hata wale wa damu wanaweza kukuvunja moyo hivi hivi kama huyo wifi yako.

Kiufupi, jali maisha yako na yeye aishi yake. kingine, usiwe utnaenda wema kwa mtu kwa kutegemea mazuri/wema kutoka kwake pia. maana kama uko hivyo utakuwa unaumia kila siku.
 
Jully wakati mwenzio anapanda maisha hadi u director we bado unakula dagaa na kuishi chumba cha kupanga?
Just curious?
 
mbona hiyo poa tu,watu wazima kila mtu alale kwake, kutembeleana na kusalimiana inatosha!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom