Wifi hotspot yenye login page

h120

JF-Expert Member
Jan 10, 2012
2,532
3,316
Habari wana tech,
Leo tufahamishane kuhusu wifi hotspot zenye login page, mara nyingi hufahamika kama captive portal, hii mifumo hutumika sana kwenye migahawa ya kisasa na mahoteli ya kisasa, na pia kuna baadhi ya ISP hutumia huu mfumo kusambaza internet via wifi.

Jinsi inavyofanya kazi;
Mtumiaji wa computer au smartphone anapo search wifi networks kama zipo utakuta baadhi ni secured kwa maana zinahitaji WEP au WPA/WPA2 key (password) na nyingine huwa open kwa maana unaweza ku connect bila kuhitaji password, Hotspot zinazotumia captive portal mara nyingi huwa open na mtumiaji huweza ku connect bila kuhitajika kuingiza password isipokuwa utakaribishwa na login page itakayotaka uingize voucher code au username na password ili uweze kutumia internet, taarifa zote zinakuwa zinahifadhiwa katika database ya server, kupata voucher codes inategemea na mtoa huduma kama ni mgawaha wanaweza kutoa kama promo code au offer baada ya kununua huduma mfano chakula, Limitation zipo nyingi inaweza kuwa time based, au volume based. Kwa msaada wa server an softwares wapo na total control kwa clients wote waliounganishwa kwenye network husika.

Hapo juu nimejaribu kuchambua ufanyaji wake kazi kwa kifupi zaidi yapo mengi zaidi ya hayo, lengo haswa la huu uzi ni kuelekezana namna ya kutengeneza wifi hotspot yenye captive portal feature kupitia PC yako yenye wifi au router. Hayo niliyoeleza hapo juu yote unaweza kufanya kwenye PC yako iwapo ina wifi, najua tumezoea kutumia wifi tethering za kawaida kwenye smartphone na pc ila kuna muda unatamani uweze ku control clients wako inakuwia vigumu kwasababu ukishaweka password tu basi hamna kingine unaweza kufanya.

Kuna software mbili tu zitakazotumika,
swali la msingi je ni nini haswa hii hotspot inaweza fanya;

1.PC yako ndio itakuwa server
2.Utaweka users kadri unavyotaka (username & password) na yeyote anaweza kujisajili bila kupata access ya internet mpaka umpe ruksa aidha kwa malipo au unavyojua wewe.
3.Unaweza ku generate voucher codes kama hutaki watumie user id
4.Unaweza control speed kwa clients wote waliokuwa connected kulingana na bandwidth iliyopo
5.Unaweza ku terminate client yeyote atakayeenda kinyume na matakwa yako
6.Unaweza block sites ambazo hutaki wavisit
7.Unaweza kuweka free site ambazo mtu asiye na voucher au user id anaweza access, idadi ni utakayo amua wewe.
8.Yeyote atakaye connect kwenye wifi yako atakutana na login page, anaweza kuingiza voucher code au user id. Voucher codes una generate wewe admin ya muda unaotaka inaweza kuwa wiki, siku masaa au dakika, na unaweza generate nyingi tu na muda wake wa ku expire unaweka kama itumike ndani ya saa au siku au ikishatumika mara moja isifanye kazi tena na mengineyo mengi.
9.Zipo feutures nyingi tu hizo ni baadhi zilizonivutia.

Kinachohitajika;
Computer ; laptop/desktop [lazima iwe na wifi, yaweza kuwa USB au built in wifi] router na access point pia zinaweza tumika.
Internet conectivity; yoyote kati ya hizi, 4G/3G/wifi/LAN etc

softwares;
Wifi creator -Hii itatengeneza virtual router kwenye pc yako
Myhotspot -Hii itafanya yote yaliyoelezwa hapo juu

wifi creator
img1.jpg

Hiyo ndiyo yatengeneza virtual router ni simple na rahisi sana kutumia.

Myhotspot
hotimg1.jpg

Myhotspot ndiyo hiyo

Login page kwa client
myhotspot_login.png

Installation na configarion ni rahisi sana kufanya kwa hiyo sintaweka steps zote nitaweka link yao hapa kwa atakaekwama apitie hapa au uliza tutasaidiana LINK.

Binafsi nimeitumia iko vizuri sana na pia login page unaweza kui customize kadri unavyotaka, kwa hiyo kwa wale mliokuwa mkiombwa wifi tethering na mnachukia mioyoni juu ya uliwaji wa MB mithili ya pampu za sheli:D:D ni wakati sasa wa ku control bando lako kadri upendavyo.
Na pia ni nzuri kibiashara kama mtu atakuwa serious na vifaa vizuri inaweza kuwa sehemu ya ujasiriamali.

Hapa chini nikiijaribu kwa kutumia PC tofauti.
 
Habari wana tech,
Leo tufahamishane kuhusu wifi hotspot zenye login page, mara nyingi hufahamika kama captive portal, hii mifumo hutumika sana kwenye migahawa ya kisasa na mahoteli ya kisasa, na pia kuna baadhi ya ISP hutumia huu mfumo kusambaza internet via wifi.

Jinsi inavyofanya kazi;
Mtumiaji wa computer au smartphone anapo search wifi networks kama zipo utakuta baadhi ni secured kwa maana zinahitaji WEP au WPA/WPA2 key (password) na nyingine huwa open kwa maana unaweza ku connect bila kuhitaji password, Hotspot zinazotumia captive portal mara nyingi huwa open na mtumiaji huweza ku connect bila kuhitajika kuingiza password isipokuwa utakaribishwa na login page itakayotaka uingize voucher code au username na password ili uweze kutumia internet, taarifa zote zinakuwa zinahifadhiwa katika database ya server, kupata voucher codes inategemea na mtoa huduma kama ni mgawaha wanaweza kutoa kama promo code au offer baada ya kununua huduma mfano chakula, Limitation zipo nyingi inaweza kuwa time based, au volume based. Kwa msaada wa server an softwares wapo na total control kwa clients wote waliounganishwa kwenye network husika.

Hapo juu nimejaribu kuchambua ufanyaji wake kazi kwa kifupi zaidi yapo mengi zaidi ya hayo, lengo haswa la huu uzi ni kuelekezana namna ya kutengeneza wifi hotspot yenye captive portal feature kupitia PC yako yenye wifi au router. Hayo niliyoeleza hapo juu yote unaweza kufanya kwenye PC yako iwapo ina wifi, najua tumezoea kutumia wifi tethering za kawaida kwenye smartphone na pc ila kuna muda unatamani uweze ku control clients wako inakuwia vigumu kwasababu ukishaweka password tu basi hamna kingine unaweza kufanya.

Kuna software mbili tu zitakazotumika, swali la msingi je ni nini haswa hii hotspot inaweza fanya;

1.PC yako ndio itakuwa server
2.Utaweka users kadri unavyotaka (username & password) na yeyote anaweza kujisajili bila kupata access ya internet mpaka umpe ruksa aidha kwa malipo au unavyojua wewe.
3.Unaweza ku generate voucher codes kama hutaki watumie user id
4.Unaweza control speed kwa clients wote waliokuwa connected kulingana na bandwidth iliyopo
5.Unaweza ku terminate client yeyote atakayeenda kinyume na matakwa yako
6.Unaweza block sites ambazo hutaki wavisit
7.Unaweza kuweka free site ambazo mtu asiye na voucher au user id anaweza access, idadi ni utakayo amua wewe.
8.Yeyote atakaye connect kwenye wifi yako atakutana na login page, anaweza kuingiza voucher code au user id, voucher codes una generate wewe admin ya muda unaotaka inaweza kuwa wiki, siku masaa au dakika, na unaweza generate nyingi tu na muda wake wa ku expire unaweka kama itumike ndani ya saa au siku au ikishatumika mara moja isifanye kazi tena na mengineyo mengi.
9.Zipo feutures nyingi tu hizo ni baadhi zilizonivutia.

Kinachohitajika;
Computer ; laptop/desktop [lazima iwe na wifi, yaweza kuwa USB au built in wifi] router na access point pia zinaweza tumika.
Internet source; yoyote kati ya hizi, 4G/3G/wifi/LAN etc

software;
Wifi creator -Hii itatengeneza virtual router kwenye pc yako
Myhotspot -Hii itafanya yote yaliyoelezwa hapo juu

wifi creator
View attachment 410554
Hiyo ndiyo yatengeneza virtual router ni simple na rahisi sana kutumia.

Myhotspot
View attachment 410555
Myhotspot ndiyo hiyo

Login page kwa client
View attachment 410556

Installation na configarion ni rahisi sana kufanya kwa hiyo sintaweka steps zote nitaweka link yao hapa kwa atakaekwama apitie hapa au uliza tutasaidiana LINK.

Binafsi nimeitumia iko vizuri sana na pia login page unaweza kui customize kadri unavyotaka, kwa hiyo kwa wale mliokuwa mkiombwa wifi tethering na mnachukia mioyoni juu ya uliwaji wa MB mithili ya pampu za sheli:D:D ni wakati sasa wa ku control bando lako kadri upendavyo.
Na pia ni nzuri kibiashara kama mtu atakuwa serious na vifaa vizuri inaweza kuwa sehemu ya ujasiriamali.

Hapa chini nikiijaribu kwa kutumia PC tofauti.

nakumbuka hii kitu nilikuwa napambana Nayo enzi za chuo. Kumbe ndo inavofanyiwa configuration. Asante Mkuu kwa elimu
 
Hizi version mpya zimeboreshwa sana, nakumbuka kipindi cha nyuma hata mimi nilihangaika sana na hizi captive portal ila zilikuwa zina buma, nilizowahi jaribu ni Antamedia hotspot hii ilikuwa inataka uwe na Ethernet port mbili kwenye PC, nyingine ni ARPminer hii ipo simple sana na haina features nyingi ila inapiga kazi vizuri.
 
Ukisha ruhusu mtu a connect kwa captive portal means tayari ushampatia yeye access ya Internet...Kitakachofata ni ku break through!

Je,hii security concern vipi?
 
Unachosema ni sahihi lakini kumbuka hapa hautakuwa na users laki moja au milioni na hivyo ni rahisi kui manage network yako, kwa clients wengi ni changamoto kidogo ila pia zipo equipment zenye firewall nzuri, ila kwa hii software hata kama client atafanya tunneling via dns au ssh utaona tu unusual traffic flow ambazo hazijifichi hivyo ni rahisi kuchukua hatua.

qwqe.jpg

Kama utaweza kui fool router au access point isionyeshe taarifa zako kwenye monitoring software hapo umewin ila vinginevyo ni ngumu kidogo. Kwa hiyo ili ufanye ku bypass captive portal bila kushtukiwa inabidi usionekane kwanza kwenye server kitu ambacho si rahisi sana.
 
View attachment 411140

Hapo nimekusoma Mkuu!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom