Wife amewaka na mimi kuhusu Valentine!

Wife amewaka na mimi kuhusu Valentine!

God bell

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2011
Posts
590
Reaction score
211
Wife amelianzisha jioni hii, anadai amenivumilia sana kila mwaka sichukulii serious siku ya valentine kumuweka mkao kumuweka mkao. Anataka kila 14th of february niwe namnunulia nguo, viatu na hereni atokee out ili ajione na yeye yuko katika wanawake wanaopendwa. ''Jamani kuna mambo mengi ya kufanya sio kukaa na kufikiria valentine day wakati kama ni kupendwa ni kila siku ijayo kwa Mungu.''ndivyo nilivyo mjibu. Basi amenunaa hadi sauti imefifia. Ndo nanyoosha miguu huku mtaani maana nimeona kuendelea kukaa hapo home kuna uwezekano wa kuzuka balaa zaidi.
 
pole kk mweleweshe taratibu kwani wanawake wana tabia ya kuchokoza na kukuangalia mpango wako nn cha msingi jitahidi mambo ya msingi yasikosekane nyumbani
 
Umenikumbusha mwaka jana siku ya valentine katika mishemishe za town jamaa kapokea simu ya mke wake, hee mwanamke si kaanza kulalamika oo sijui hunipendi sijui nini yaani maneno kibaaao, yule jamaa ata hajui nini kinaendelea kamuuliza wife kwani nimefanyaje mpka unasema ivo? Shem kajibu kwani hujui kama leo ni valentine? Jamaa limemtoka lile fyonyo balaa thn kakata simu. Sio kila mtu anaona valentine ni muhimu kivile
 
watoto wa .com wanashida sana kila kitu wantaka wacopy na kupaste
 
Mwambie Valentine si sheria aache utoto kama haupo romantic siku zote how can u magically turn into a Romeo character siku moja kwa mwaka
Mpende how u know best kama unavyompenda kila siku

Kama ni kumpenda nampenda sana siku zote....hili la valentine sijui kalitoa wapi. Halafu nilikuwa sijui kama kesho ndo siku yenyewe kwani mambo ni mengi katika kuhakikisha mpango mzima wa kuitunza familia umekaa sawa.
 
Kama ni kumpenda nampenda sana siku zote....hili la valentine sijui kalitoa wapi. Halafu nilikuwa sijui kama kesho ndo siku yenyewe kwani mambo ni mengi katika kuhakikisha mpango mzima wa kuitunza familia umekaa sawa.

Obviously it's everywhere kwenye media and all over.....imeshakuwa planted in our brains as if our very love life depends on it
Just muelimishe though
 
Angaalia kale kwa wimbo ka rich Mvoko kasije kukuta...............kuchapiwa siri ya ndani.......
 
pole kk mweleweshe taratibu kwani wanawake wana tabia ya kuchokoza na kukuangalia mpango wako nn cha msingi jitahidi mambo ya msingi yasikosekane nyumbani
Hapa ndio pa muhimu sana. Jambo la msingi sana hapa ambalo halipaswi kukosekana ni wewe mwenyewe Hakikisha mnashinda wote nyumbani au mnatoka out sio umwache uende out peke yako utamfanya awaze vibaya kuwa labda yuko "valentine" mwingine unayemfuata huko.Labda huyo ndiye kanunuliwa nguo na viatu.
 
mkuu wanawake ndo zao...sasa wewe kesho mpe hela akanunue ivo vitu afu jioni mwambie sijiskii kutoka..tuone ka atakufa...maana wanapenda sana mashindano hawa viumbe..
mimi binafsi mpaka sasa tulikwaruzana majuzi..kisa kakutana na ex wangu mara mbili mitaa karibia na ofisini kwangu..bass ndo kafulaa huyo wakat ata mie sijawasiliana na huyo ex kama mweez sas..leo nimemtumia hela akale na huyo ex wangu anayemtaja taja...naona mtu anagwaya..ooh tutoke..nimegoma..
 
Ndo maana ndoa zinakuwa ngumu, mkishaoa huduma zinakatwa
kweli samaki anapewa chambo akiwa anavuliwa tu
baada ya hapo ooh mambo mengi ooh maisha magumu
kama maisha magumu achana nayo fan ya mambo mengine....
 
Nishasema kila siku kwangu ni valentine wala hata sijui inasherehekewaje hii siku. Unaweza ukakomaa na siku moja eti ndo yenye furaha badala yake ukakosa furaha mwaka mzima.
 
Siku zote huwa unamjali jali na hivyo vitu anavyodai au ndio kanga zimepauka kama zilimwagiwa jiki na viatu fundi wa viatu kavichoka?

Nwy kama unaweza mpe tu maana baadhi ya wanawake utoto tu unawasumbua. Hapo anafikiria wenzake waki'brag yeye atabakije kuwasikiliza tu bila yeye kushiriki. Mpe nae akaringishie marafiki na wafanyakazi wenzake.
 
Mwenyewe kesho atakuwa ofisini busy na mimi pia. Sasa sijui hivyo vitu atavivaa mda gani.
 
Back
Top Bottom