Why Rwanda draws the ire of the powerful

Why Rwanda draws the ire of the powerful

Naona Vita ya maneno kati ya Kagame na Interahamwe imehamia JF!!
 
Naona Vita ya maneno kati ya Kagame na Interahamwe imehamia JF!!

Umenena mkuu. Hii vita ni kati ya Interahamwe kama Mokala1989 na Watu wanaomtetea Kagame. Si kwa sababu nyingine bali ni kutokana na kujua historia ya Rwanda ambayo kama mnavyojua, mauaji ya kimbari yalianza kutokana na media ya rwanda wakati huo ambayo ndio iliyokuwa ikichochea mauaji hayo. Sasa tunajua tukiwaachia watu kama Mokala1989 wakaendelea kuwanyunyizia sumu watanzania ambao tumeishi nao kama majirani kwa miaka mingi, mwishowe historia inaweza ikajirudia. We cannot allow that to EVER happen again.
 
nadhan aliyekuja na idea kuhusu kua na forum kuhusu rwanda big up we need it... i personally think wa tz na wenzetu wa rwanda we do not have the big issue to fight the only way issue itakuwepo iwapo kweli M23 ni jeswhi la rwanda bcoz nadhan rwanda hawatakubali wa tz wawaue askari wao ambao wameji ni siduise kama M23...... otherwise peace and love
 
Binafsi huwa naona uchungu sana kuona binadamu anapoteseka sana au kufa bila hatia........ na naumia zaidi nikiona mateso au vifo hivyo vya binadamu asiye na hatia vinasababishwa na binadamu......... inaniuma sana.... na mara nyingi nakuwa na mawazo yasiyofaa (nakiri wazi) ''kuwa bora binadamu asiwepo juu ya uso wa dunia kama mambo ya ukatiri anamfanyia binadamu mwingine...... au anamtawala binadamu mwingine kwa kumuumiza (kwa hasara ya mwingine)......

Na ndiyo maana mimi kwa dhat kabisa nitamuunga mkono rais Kikwete popote...... kuhusu wazo lake la kukaa pamoja au kufanya mazungumzo na waasi.... hii ni njia ya kiungwana na ya KIMUNGU kwa maana inawaleta pamoja watu waliohasimiana na kuongea mambo mengi ya msingi ya kwa nini walihasimiana na nini kifanyike ili hali hiyo isijirudie tena..... Kukataa kuongea na adui wako ni kuzidisha uadui na matokeo yake ni madhara zaidi....

UMENENA VYEMA KABISA...kama sijasahau FDLR inaundwa na wanajeshi walokuwa wanajeshi wa serikali ya Rais Marehemu Juvenal Habyarimana na Interahamwe walopanga na kutekeleza Mauaji ya kimbari dhidi ya WATUTSI ya 1994. Madai yao ni ya muda mrefu kanzia miaka ya 1950 yakiwa hasa ni kufuta kabila la Watutsi katika nchi ya Rwanda---ni madai ambayo kimsingi hayawezi kutekelezeka kwa kukaa meza moja....madai yanayoweza kutekelezeka kwa kukaa meza moja ni kama yale kati ya M23 na serikali ya Congo,ADF na serikali ya uganda,FNL na serikali ya Burundi, nk...hawa madai yao ni ya kiutawala power sharing nk...yanatekelezeka na wanaweza kukaa meza moja na kuyamaliza kama ilivokuwa kwa CCM na CUF zanzibar.....lakini kwa hili la Rwanda kidogo napata ugumu jinsi ya kukaa meza moja wakati madai ni kama nilivoeleza hapo juu... soma hizi amri 10 za wahutu kama zilivotangazwa na kuandikwa na Kangura news wakati wa maandalizi ya mauaji ya kimbari ...........Hutu Ten Commandments - Wikipedia, the free encyclopedia

TUDUMISHE amani
 
Inawezekana ni kweli.... lakini usiogope maneno hayo..... maana sidhani Wahutu wote wanakubaliana na hizo amri 10..... ni kitu cha kufikirika.... (ZIMEKAA KISHARI HIVI KWAMBA HATA ANAYEPASWA KUZISHIKA NA KUZITEKELEZA NI MZIGO KWAKE...... SI MAISHA YA RAHA).... kwa maana mpaka sasa tuna ushahidi wa kutosha kabisa unaoonesha kuna mafungamano ya kijamii kati ya Wahutu na Watutsi...... wameoleana...... wamezaana....... hizo amri si kwa wananchi wa kawaida..... ila ni kwa wanasiasa....... ambao mara nyingi mimi (sijui kama nakosea) nawaita wafuasi wa shetani...... sababu kubwa ni kwamba hamna kweli ndani yao...... ndiyo yao haitegemeki...... na siyo yao pia usiiamini sana...... mara nyingi sana wametenda kwa hila kwa kukusudia.....

Hivyo bad mimi ni muumini wa kukaa meza moja...... muda mrefu umepita na kizazi hiki sidhani kwamba kutang'ang'ana na historia ambayo haijengi mstakabali mzuri wa taifa lao..........

Wasiwe kama wendawazimu fulani ambao kwa maslahi yao binafsi wanaanza kutumezesha ubaguzi kati ya Tanzania bara na Tanzania visiwani..... Miaka yote watu waliozaliwa tangu 1964 wanaona visiwani ni kama bara na wana uhuru wa kutembea upande wowote...... lakini limeibuka kundi (siui kwa manufaa ya nani) linataka kuwaaminisha vijana kuwa Tanzania visiwani na bara si ndugu.... yaani mmi naona kama wewe vile umelelewa kwenye familia yenu kwa mapenzi makubwa kwa miaka yote mpaka na wewe unakuwa na familia...... halafu mama yako anakuambia huyu aliyekulea si baba yako.... kuna baba yako sehemu fulani....... huko ni kuchanganyana kwa kiasi kikubwa..... sasa ina maana wale shangazi zako uliowazoea (yaani dada za baba huyu aliyekulea) uanze kuwaona si ndugu zako.....binamu zako, baba wadogo n.k.... wote hao uanze kuwafikiria tofauti.... huo ni ushetani wa hali ya juu.... Hicho ndicho wanachokifanya wale wanaotaka kujitenga toka muungano...... HILO NALIONYA (KWA SAUTI KUU)..... WANAFANYA HIVYO KWA HASARA YA UNDUGU WETU, JAMII YETU NA TAIFA LETU ..... WAKUMBUKE (WANASIASA) KUWA MADARAKA WANAYOYATAKA HAYASHINDI MAMBO HAYA MATATU NILIYO YATAJA.... WENYEWE WATAPITA LAKINI HIVI VITADUMU.....
 
Back
Top Bottom