Why NOT Tanzanians(Africans)?

Big Dy

JF-Expert Member
Dec 23, 2015
475
561
Hello JF

Well over the past holiday (x-mass & new year) nilipata chance ya kuzungumza na moja ya alie kua potential figure katika nchi yetu ila baada ya kustaafu sasa anajishughulisha na biashara in fact amewekeza kwenye kiwanda huko kaskazin.
Kitu ambacho tulikua tunaongea ambacho nimekua nikikiria from that day ni KWANINI WA TANZANIA/AFRICA HATUWEZI KUENDELEZA BIASHARA/VITEGA UCHUMI FOR YEARS?. Hili swali nimekua nikilifiria sana kwanini sisi hatuwezi kuendesha biashara zetu binafsi(Family business) kama vile viwanda, maduka or hata kilimo ukilinganisha na wenzetu Asians like Indians, Chinese n.k ambao unaweza kuta biashara nyingi walizo nazo sasa chimbuko lake ni tangia mababu zao walio anzisha na kufanya kurisishana vizazi hadi vizazi.
Nimeona nilifikishe hili jambo kwa wadau wenye ujuzi zaidi na tafakuri zaidi yangu nadhani inaweza kusaidia huko mbeleni kwa vizazi vyetu.
 
Nadhan ungeweka hapa hicho mlichokiongea na huyo alikua potential figure.

Sababu kubwa na ya kimsingi biashara zetu sio shirikishi. Biashara zetu nyingi anaejua nini kinaendelea ni baba tu, mama na watoto hawashirikishwi hata kidogo na hii ni kutokana na mila na destuli zetu waafrika kwamba mama hatakiwi kujua kipato sahihi cha baba au hatakiwi kushirikishwa sbb wakijua wanaweza kutubana katika matumiz, au tuna amini wanawake wanaweza kufuja/kuiba na kwenda kufanya maendeleo kwao au hata kukuua ili amiliki biashara hiyo. Vile vile Kwa watoto tuna amini wataiba na kufanya matumiz ya hovyo. Mbaya zaid licha ya kutoishirikisha familia pia hatuna utamaduni wa kumwandaa successor wa kuendeleza biashara pale inapotokea tumefariki au kupata matatizo yatakayotufanya kutoweza kuindesha biashara hiyo.
Inapotokea tumepoteza maisha, mama na watoto hawatakua na uwezo wa kurun biashara zetu sbb hawakushirikishwa kwa chochote zaidi ya kula tu na sio kutafuta na hapo biashara mara nyingi ufa. Jarib kuangalia mitaani kwetu utagundua baba akifa tu na biashara ufa, alaf tunakimbilia kulaum watoto wanafuja hela za baba yao.
Angalia life style ya hayo mataifa uliyoyataja, ni watu wanaopenda kuambatana na familia zao ktk kila jambo, ndo maana unakuta watoto wao pamoja na mama wanajua a to z ya nini baba anachofanya na wanashirikishwa kadri ya umri na elimu zao mpaka wanakua na uwezo wa kuwa saidia wazazi wao.
Pia wenzetu upendelea kutoka out na familia zao yaani baba, mama na watoto wao hata hapa bongo hayo ndo maisha yao jaribu kuwachunguza. Hii inaongeza ukarib sana na pia inasaidia ktk malez bora ya famili.
Wkt kibongo-bongo ni vigumu kumkuta baba katoka na familia yake yote, mara nyingi tunakua na michepuko ambapo msingi wake umejengwa kwenye matanuz sbb pesa ipo.
Je unatoka out mara ngapi na familia yako ukilinganisha na unavyotoka na washkaji?
Je ua unainjoi kuwa nao au imebidi sbb umebanwa?
Tuanzie hapa kuishirikisha familia ktk ishu zetu na tuwe nao karib kuliko ilivyo sasa alaf tuone kama biashara zetu zitapotea pindi wakina-baba tutakavyorudisha namba.
 
Back
Top Bottom