Wakuu Kuna ishu moja inanitatiza...Tumekua tukisikia watu mbalimbali Wakitanguliza Jina la Cheo kabla ya Majina yao....kama vile Balozi, Dr., Prof..sasa nauliza tuna viongozi wengi wamepitia Ualimu lakini mpaka leo ni Mwalimu Nyerere pekee ndio alipenda kuitwa kwa kutanguliza jina la Mwl...Sasa swali ni kwamba hawa viongozi wengine hawapendi au hii imekaaje?? Just curiosity tu!!
Alikataa with a straight face kuitwa majina mengine yoyote ya Kumkweza au kumwabudu, na akasema yeye ataitwa Mwalimu tu..not Mheshimiwa, Mtukufu, Dr...etc
Zebaki,
Kuna huyu waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Anne Kilango Malecela na hata First Lady wetu, Bi Salma Kikwete. Ni walimu hawa. Kuna wengine kibao