mulwanaka
JF-Expert Member
- Feb 19, 2017
- 5,262
- 12,837
- Thread starter
- #101
Naona majibu malefu kama kawayda ya watu wa wauongo wanavo fanya eti unaeleza neno "la nabbiyu baada"hahaha ..... kwa mtu yoyote mwenye basic knowledge ya kiarabu hawezi kutafuta maana nyingine ya hilo neno "hamna mtume baada yangu".........ila kwasabb nyie majahiliya Qadiani au Ahmadiyya kazi yenu ni kupotoshwa ukweli endelea tu.......waIslamu tulisha amka hampati wafuasi , endeleani kutoa soda za bure na vitafunwa kununua watu.Mimi ninakubaliana kabisa na hiyo hadithi na ipo wazi kabisa na haikomeshi utume kabisa bali inaendekeza utume na wala haihitajiki akili kubwa kuielewa hiyo hadithi japo maneno ya mwisho yanayosomeka; لا نبي بعدي (laa nabiya ba'adii) yanahitaji maelezo kidogo, na hapa ndipo kwa matatizo kwa Waislamu wengi, kwani hawasomi hadithi na Qur'an kwa tafakur, Qur'an Unasema Utume inaendelea utawaona baadhi ya Waislamu wakisema Mtume Muhammad (saw) ni wa mwisho kuja--- sasa hawaoni kuwa hapa wametengeneza ikhtilafu ndani ya Qur'an bila kujua.
Neno ba'adi (بعدي) linazo maana 3, 1-- in my absence, 2--after me, 3-- Contrary to me., maana kubwa iliyozoeleka ni #2 , sasa tuone maana nyingine ya neno بعد (ba'ad) ilivyitumika ndani ya Qur'an :-
تلك ايات الله نتلوها عليك فبأي حديث بهد الله و اياته يومنون---- yaani; Hizi ni aya za Allah tunakusomea kwa haki; basi ni hadithi gani watakayo iamini KINYUME na Allah na aya zake? (45:6) Qur'an .
Hapo sasa utaona neno ba'ad likiwa na maana ya "kinyume", hivyo sasa maneno لا نبي بعدي maana yake ni hakuna nabii kinyume nami au hakuna nabii atakaye kwenda kinyume na mimi, ukitafsiri hakuna nabii baada yangu utaleta ikhtilafi ndani ya Qur'an kwani kuna aya nfano (7:35) inasema mitume watakuja kuwasomamea/kuwafundisha watu aya za Qur'an.
Sasa nije kwa hadithi yenyewe, kwenye maneno mengine انا جاتم النبيين yaani; na mimi ni khatam an nabiyyin, neno khatam maana yake ni Muhuri au mbora, hapo sasa tutatafsiri; "na mimi ni mbora wa manabii", hivyo utaona hadithi nzima haijafunga utume/unabii kabisa bali ni tafsiri mbovu ndizo zinataka kutuaminisha kwamba utume umefungwa kitu ambacho ni kinyume na Mafundisho ya Qur'an.
Sasa nije kwenye hadithi yote, Mtukufu mtume (saw) alikuwa anajua fika katika umma wake watatokea Waongo 30 na kila mmoja atadai kwamba yeye ni mtume lakini hakusema kwamba KILA mtu atakaye dai utume ni Muongo!!---- tena kaweka hadi idadi ya Waongo 30 kwa maana kwamba Nabii mkweli anaweza kuwa wa 31, kifupi ni kwamba hadithi inataja waongo 30 na haijasema kwamba Kila atakayedai unabii ni Muongo!!, na hii ni tahadhari ili akitokea nabii mkweli tuweze kumtofautisha na muongo, in that regard The holy prophet was very brilliant messenger of Allah.
Hebu chukua mfano huu; Baba anaondoka nyumbani na anamuaga mwanaye huku akimtahadharisha kwamba; "Mwanangu usiache milango wazi nimesikia watakuja wezi kuiba hapa" ----- je kila mtu atakaye kwenda hapo nyumbani atakuwa ni mwizi???!!---- common sense inasema sio kweli kwamba kwamba kila atajayefika pale nyumbani atakuwa miongoni mwa wale wevi.
Hata hivyo Wataalamu wa hadithi waliifanyia kazi hiyo hadithi na hebu sikia walichosema:-
هذ الحديث ظهر صدقه فانه لوعد من تنباء من زمنه صلى الله عليه و سلم الى الان لبلخ هذ العدر و يعرف ذالك من يطالع التارايخ
(اكمل الاكمل جلد مصرى )
Yaani; Hadithi hii imedhihiri ukweli wake, maana lau wakihesabiwa waliodai utume toka wakati wa Swalallahu aleyhi wa salam (mtume mtukufu saw) mpaka sasa itatimia idadi hii, na jambo hili analijua anayesoma historia. (Ikmal alikmal kutoka Misri).
Aliyeandika hicho kitabu alifariki mwaka 828 Hijriyya.
Kwa mujibu wa Qur'an hata mtukufu mtume (saw) na mitume wengine walishambuliwa kwa matusi na kejeli kutoka kwa wapinzani, nawe umejipambanua kushika tabia ya wapinzani wa mababii kwa kutoa kejeli dhidi ya Hadhrat Ahmad (as) na hii ni ishara ya ukweli wake watu wema wanaelewa lakini wapinzani Allah huwazidushia kiburi, chuki na hasira nyoyoni mwao.
Omba toba na msaada kwa Allah ili uutambue ukweli kiburi na majivuno na kauli chafu dhidi ya Hadhrat Ahmad (as) itakaribisha hasira ya Allah juu yako, ni Allah pekee anayeweza kumuongoza mtu mimi nafikisha ujumbe tu basi omba msaada kwake kwa unyenyekevu na subira na swala bila shaka Allah atakuongoza.