Why do most girls or women want to settle with a ready made man?

joshydama

JF-Expert Member
May 10, 2016
4,623
5,039
Asalam aleykum wana MMU!
Kama kichwa cha habari kinavyojiekeza hapo juu.

Ningependa kujua ni kwanini wasichana au wanawake wengi wanapenda waolewe au kutoka na watu waliofanikiwa kimaisha mfano mwanaume mwenye kazi nzuri, amejenga na ana usafiri wake( chombo cha usafiri) au Gari na hela fulani ya kubadilisha mboga.

Je ni uoga wa maisha unasababisha mnawapenda wanaume wenye mafanikio au hampendi mpate shida za hapa na pale?

Hamuwezi kumpenda mwanaume ambaye hana kitu chochote mwisho wa siku mkaunganisha nguvu na jitihada kwa pamoja mkapambana mwisho wa siku mkafika mnapopataka?

Karibuni kwa michango!
 
SIDHANI KAMA WEWE UNGEKUWA MWANAMKE UNGEPENDA KUOLEWA NA MTU AMBAYE MAISHA YAKE HAYAELEWEKI.NI NATURE YAO MKUU
Sijamaanisha kwamba maisha hayaeleweki Mkuu.

Ukisema maisha hayaeleweki inamaana ushapoteza dira ya maisha kabisa na haujishughulishi wala nini.

Upo katika utafutaji lakini hauna hela nyingi sana,gari wala wala nyumba!
 
Hivyo ndivyo inavyotakiwa kuwa, hata ktk maandiko Mungu alimpa Adam kazi ya kufanya na chakula cha kuprovide ndio akampa mwanamke. Nikuulize tu, utapendaje mambo magumu, yaani unapenda kitu kibaya wkt kizuri kipo?
Sawa!

lakini vitu vizuri vinagharama sana Mkuu.

Kuna wadada fulani niliwashuhudia ulikuwa ukienda kuwachumbia wanakuuliza una vigezo gani? Na kitu gani kimekupa ujasiri wa kuja kunichumbia?
Wao walikuwa wanataka wanaume wenye funguo tatu;

•Funguo ya nyumba
•Funguo ya gari.
•Funguo ya ofsini

Walikuwa wanaringia uzuri wao lakini mpaka sasa hivi wapo nyumbani wanasaka wanaume hatari na wapo kutoa mahari wenyewe.
 
Sijamaanisha kwamba maisha hayaeleweki Mkuu.

Ukisema maisha hayaeleweki inamaana ushapoteza dira ya maisha kabisa na haujishughulishi wala nini.

Upo katika utafutaji lakini hauna hela nyingi sana,gari wala wala nyumba!


Nimekusoma mkuu
 
Kila la heri kwao japo najua sio wote ..wafanye ile inaitwa sorting process ...huyu ana hela, huyu hana masikin maisha yake hayaelewek siwez kua nae,namuondoa huyu kwenye list naenda kwa jamaa mwenye hela gari na kaz nzuri na aliejenga.
Pia inabidi wakiwa wanafanya hivyo nao wajiulize na kujitathimini kama wana hivyo vitu?
 
Back
Top Bottom