Wacha1
JF-Expert Member
- Dec 21, 2009
- 16,681
- 8,241
Kwa nini members wengi wanajadili sana maswala ya Rwanda, Burundi, Kenya, Somalia kuliko mambo yanayowahusu hususan yanayotokea ndani ya Tanzania?
Pamoja na kuwa member wa hii forum kwa muda mrefu nimegundua kwamba Watanzania wachangiaji wengi wa hii Forum wanapenda sana kuongelea yale yanayotokea kwa majirani wachilia, Somalia et al. Hawa ndio tunasema ni wasomi ambao huenda wakawa na mawazo ya kuiondoa Tanzania kwenye dimbwi la umasikini na kuwavusha wengi ambao hata hawafahamu JF. Je ni ukweli usiopingika kwamba wengi wao maendeleo wanayoyaongelea ni yale ambayo wameyaona kwenye luninga tu? Kwenye vitabu na sinema et al. Wengi wao hawajasafiri kwenye nchi ambazo kweli ni ishara ya maendeleo. Wengi wanajaribu kulinganisha jinsi nchi yetu inavyotakiwa kufanya shughuli zake lakini wanashindwa kuona kwamba hivi viinchi vya Kenya, Rwanda, Burundi, Congo, Somalia et al ni failed states.
Tujivunie kufuata mifano ya nchi kama Sweden, Norway, UK, USA, Singapore, Japan, Canada etc. Demokrasi ya Uingereza au USA ni Zaidi ya miaka 400. Huko ndiko tunaweza kuona vipi and how we can develop na kututoa hapa tulipo. Kuangalia nchi ambazo ni changa ambazo wao wanauana kama kima au tumbili ni mapungufu kwa wale ambao wanafahamu Tanzania inahitaji chachu ya aina gani ili iendelee. JF kama kweli tunataka tuwe sauti inayosikika tuache ufinyu wa fikra na tuwe wachambuzi kweli sio mambo ya fitina ya kujadili kanga au vitenge. Hayo tuyaache kwenye sports na burudani. Tunapoingia kwenye mambo ya msingi ya kizazi kijacho cha Tanzania tuwe more than serious kuonyesha kwamba tunafahamu nini tunachokiongelea. Tumekuwa taifa kubwa na ni lazima tuwaenzi wale waliolipigania taifa hili kwa udi na uvumba kutoka kwenye minyororo ya wakoloni. Tulikuwa na kina Mkwawa, Kinjekitile, Mirambo, Chabruma, Seuta, Nyerere, Sokoine et al. Tutakuwa hatuwatendei haki watoto wetu na kizazi kijacho kwa urithi tulioachiwa na kuacha mafisi machache ya ndani na nje kuja kujineemesha kwa jasho la walipa kodi wa Tanzania. Nafahamu wengi wamesoma kwenye nchi hizo za magharibi/mashariki na wana michango mikubwa tu lakini wanajificha hawataki kuonekana humu na kutoa duku duku zao. Tanzania ni kwa ajili ya kizazi kijacho bring in your good ideas.

Last edited: