Kwanini Machali na Mkomali hawajawahi kuisema vibaya Chadema?Moses Machali na Felix
Mkosamali walikuwa wanachama na viongozi waandamizi wa CHADEMA hadi
uchaguzi mkuu wa 2010 unakaribia kufanyika. Wote wawili waliondoka CDM
na kujiunga NCCR walikogombea ubunge na kushinda. Ni sababu zipi
zilizowafanya kuhama CDM na kujiunga NCCR? Sera mbovu za CDM, au
walitofautiana na viongozi wa CDM? Kushinda kwao ubunge kulitokana na
ushawishi wao (nguvu yao) binafsi, nguvu ya chama cha NCCR majimboni
mwao, au kuna nguvu nyingine tofauti na hizo? Hali ya CDM kisiasa
majimboni mwao ikoje baada ya wao kondoka na kushinda ubunge wakiwa nje
ya CDM?